Friday, May 31, 2013

MAADHIMISHO YA WIKI YA UNYWAJI MAZIWA KITAIFA MKOANI RUVUMA YAFANA, MKUU WA MKOA ASISITIZA WANANCHI KUWA NA MAZOEA YA KUNYWA MAZIWA

 

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu, akizindua wiki ya unywaji wa maziwa kwa kuonyesha mfano wa kunywa maziwa, ikiwa ni njia moja wapo ya kuhamasisha Wananchi wa mkoa huo kujenga mazoea ya kunywa Maziwa. Maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya Manispaa ya Songea.
 



Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said  Mwambungu akikagua banda la maonyesho ya bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na maziwa katika sherehe ya uzinduzi wa wiki ya maziwa ambazo kitaifa zimefanyika mkoani Ruvuma. Kulia ni Dkt. Ruth Rioba Mwenyekiti wa Bodi ya Maziwa Taifa.
 
Mwambungu akiendelea kupokea maelezo juu ya matumizi ya bidhaa zinazotengenezwa kwa maziwa alipokuwa akikagua bidhaa zilizoletwa na wazalishaji na wasindikaji wa maziwa.






 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said  Mwambungu (aliyeshika maiki) akitoa nasaha kuhamasisha unywaji wa maziwa kwa Wananchi wa mkoa huo ili waweze kujenga afya zao.  Maadhimisho hayo yalifanyika katika uwanja wa Manispaa ya Songea ambapo mkoa wa Ruvuma una Ng`ombe 371,000 kati yao wa maziwa ni 12,032  ambao huzalisha lita 96,256 kwa mwaka.


 
Dkt. Ruth Rioba Mwenyekiti wa Bodi ya maziwa taifa, akifafanua jambo juu  ya kuleta maadhimisho ya wiki ya maziwa mkoani humo, katika uzinduzi wa wiki ya maziwa uliofanyika viwanja vya Manispaa ya Songea.
 
Viongozi mbalimbali wa serikali, asasi, taasisi nao walishiriki katika uzinduzi huo.
 







Ng`ombe wa maziwa wakiwa katika banda maalumu katika viwanja vya Manispaa ya Songea katika eneo ambalo maadhimisho hayo yalifanyika na kilele chake kitakuwa Juni Mosi mwaka huu.



No comments: