Wednesday, April 27, 2016

MATUKIO KATIKA PICHA SIKU YA BONANZA LA VIJANA WA MBINGA KUELIMISHA RIKA NA USAFI WA MAZINGIRA MJI WA MBINGA MKOANI RUVUMA

Vijana wakishiriki katika zoezi la usafi, kwenye eneo la soko la wakulima lililopo katika Halmashauri ya mji wa Mbinga mkoani Ruvuma siku ya maadhimisho ya bonanza la vijana wa Mbinga kuelimisha rika na usafi wa mazingira.

Wanabonanza wakiwa katika picha ya pamoja, wakati wakijiandaa kukabidhi baadhi ya vifaa vya kufanyia usafi kwa wafanyabiashara wa soko la wakulima lililopo mjini hapa.

Upande wa kushoto, Baraka Mwabulesi ambaye ni Mwenyekiti wa bonanza la vijana Mbinga akikabidhi baadhi ya vifaa vya kufanyia usafi kwa mmoja kati ya wafanyabiashara waliopo katika soko la wakulima mjini hapa.

Kutoka kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya mji wa Mbinga, Oscar Yapesa naye alishiriki kikamilifu katika zoezi hilo la kuhamasisha wananchi wazingatie masuala ya kufanya usafi katika mji huo, ambapo hapo alikuwa akikabidhi sehemu ya vifaa vya kuhifadhia taka (dust bin) kwa wafanyabiashara wa soko la wakulima lililopo Mbinga mjini. (Picha zote na Gwiji la matukio Ruvuma)

No comments: