Wednesday, March 8, 2017

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI: ANAHITAJI MSAADA WAKO ILI AWEZE KUTEMBEA VIZURI


Beatrice Ndomba, akiwa bado hajapata tatizo la ulemavu wa miguu.
Na Albano Midelo,
Songea.

HUJAFA hujaumbika, Beatrice Ndomba (24) pichani, alizaliwa akiwa na miguu yake yote miwili hadi alipomaliza kidato cha nne na kuanza kusoma Stashahada ya uhasibu mwaka wa kwanza mkoani Mbeya 2014.

Aidha akiwa huko ndipo alipatwa na ulemavu wa viungo baada ya kukatwa miguu yake yote miwili.

Beatrice hivi sasa anaishi mtaa wa Ruhuwiko kanisani, katika Manispaa ya Songea mkoa wa Ruvuma na ndoto zake za kuwa Mhasibu zimefifia.

Mwaka jana alipata mafunzo ya ufundi kushona, kwa hiyo amejiajiri kama fundi cherehani na kwamba hivi sasa anahitaji msaada wa miguu bandia, ili aweze kutembea na kuendesha shughuli zake za kujitafutia ridhiki kama Watanzania wengine.

Beatrice ni mtoto yatima, anaishi na wadogo zake wawili, ukiguswa na tatizo hili unaombwa kumchangia kiasi chochote kile ili aweze kununua viungo bandia vyenye ubora kwa kuwa alivyonavyo sasa vinamuumiza miguu na hawezi kutembea vizuri.


Mawasiliano yake anapatikana kwa simu namba 0766 642634 au 0673 054535. 

Kadhalika anawashukuru wote ambao wamemsaidia kutoka ndani na nje ya nchi hivyo kufanikiwa kuishi kwa matumaini baada ya kununua baiskeli ya kutembelea wenye ulemavu (Wheel chair), kununua cherehani mbili na kusoma chuo cha ufundi Peramiho.

No comments: