Tuesday, March 28, 2017

WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUUNDA CHAMA KITAKACHOTETEA MASLAHI YAO

Katibu Mkuu wa CHODAWU, Said Wamba akizungumza na Waandishi wa habari juu ya Warsha ya tafiti kwa wafanyakazi wasio katika sekta rasmi.
Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo wakifuatilia kwa makini hotuba ya Katibu Mkuu wa CHODAWU, Said Wamba.
WITO umetolewa kwa Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini kuunda chama chao cha Wafanyakazi ambacho kitaweza kutetea maslahi yao katika kazi.

Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta isiyokuwa rasmi (CHODAWU), Said Wamba alisema hayo alipokuwa akifungua Warsha juu ya tafiti kwa wafanyakazi hao Jijini Dar es Salaam.

“Waandishi wa habari wamekuwa mstari wa mbele katika kutetea maslahi ya wafanyakazi wengi hapa nchini, lakini cha kushangaza mpaka sasa hawana chama chao ambacho kinaweza kuwatetea pindi wanapopata matatizo na wanapohitaji kupanga maslahi yao”, alisema Wamba.

Vilevile alipongeza watu wengine ambao wamekuwa wakidharau wafanyakazi wa ndani ambao wanachama chao ambacho kina watetea, lakini wengi wao wamekuwa wazito kujiunga.

Kufuatia hali hiyo ametoa wito kwa wadau wote na watu ambao wanafanya kazi katika sekta isiyorasmi hapa nchini, kujiunga katika vyama vya wafanyakazi ili waweze kupata maslahi yao kwa wakati bila kuwepo usumbufu wa aina yoyote ile.

No comments: