Monday, May 8, 2017

MAKAMU WA RAIS AONGOZA WATANZANIA KUAGA MIILI YA WANAFUNZI WALIOFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI MKOANI ARUSHA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa zoezi la kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu wawili na pamoja na dereva mmoja wa shule ya Lucky Vicent uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha.


Jeshi la Wananchi(JWTZ) wakiingiza miili ndani ya uwanja kwa ajili ya kuombewa pamoja na kuagwa leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akitoa pole kwa ndugu na jamaa wa marehemu waliofika katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha kwa ajili ya kuaga miili hiyo.

Miili ya wanafunzi 32, walimu wawili na pamoja na dereva mmoja wa shule ya Lucky Vicent ikiwa katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha kwa ajili ya kuombewa pamoja na kuagwa leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akitoa heshima za mwisho kwenye miili ya wanafunzi 32, walimu wawili na pamoja na dereva mmoja wa shule ya Lucky Vicent katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwafariji ndugu na jamaa wa marehemu waliofika kuaga miili ya ndugu zao leo katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha.

Baadhi ya viongozi mbalimbali wa Kiserikali na chama wakiwa kwenye uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha wakati wa kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu wawili na pamoja na dereva mmoja wa shule ya Lucky Vicent.

Wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent wakiwa kwenye majonzi wakati wa kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu wawili na pamoja na dereva mmoja wa shule ya Lucky Vicent katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha.


Baadhi ya wakazi wa jiji la Arusha wakiwa katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha kwa ajili ya kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu wawili na pamoja na dereva mmoja wa shule ya Lucky Vicent waliofariki kwenye ajali.
Na Mwandishi wetu,

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Mei 8 mwaka huu ameongoza mamia ya wananchi mkoani Arusha na mikoa jirani katika kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu wawili pamoja na dereva mmoja wa shule ya Lucky Vicent Jijini Arusha katika uwanja wa Shekh Amri Abeid ambao walipata ajali kwenye eneo la Rhotia, wilayani Karatu mkoani humo.

Katika hotuba yake kwa wananchi hao waliojitokeza katika tukio hilo la kuaga miili hiyo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Pombe Magufuli, Makamu huyo wa Rais aliwahakikishia waombolezaji wote kuwa serikali ipo pamoja nao katika kipindi hiki kigumu chenye majonzi mazito kwa kuondokewa na wapendwa wao.

Makamu huyo wa Rais alihimiza wananchi wote hapa nchini kuungana pamoja katika msiba huo uliotokea, na kuwafariji wafiwa hasa kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu wote mahali pema peponi.

Pia aliagiza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Jeshi la Polisi nchini, walimu, wazazi na walezi wote kuwa makini katika kuhakikisha kwamba sheria za usalama barabarani zinazingatiwa kwa kuchukua hatua stahiki ya kulinda watoto hasa wanapotumia vyombo vya moto kwenye shughuli zao za kimasomo.

Alisema kuwa hatua hiyo endapo itazingatiwa itasaidia kwa kiasi kikubwa kuepusha matukio ya ajali ambayo yanaweza kuzuilika kote nchini.

Makamu wa Rais amewataka madereva nchini kuzingatia sheria za usalama barabarani na waache kutumia pombe na dawa za kulevya ili kuepukana na ajali ambazo zinagharimu maisha ya wananchi.

Kadhalikja alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Kenya, Uhuru Kenyatta na Wakenya kwa ujumla kwa kuungana na wananchi wa Tanzania katika msiba huu uliotokea.

Katika kuaga miili ya wanafunzi hao katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha, Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Kenyatta amewakilishwa na Waziri wa Elimu wa nchi hiyo, Fred Matiang’i.

Ibada na dua ya kuaga miili hiyo, imehudhuriwa na mawaziri mbalimbali akiwemo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mohamed Aboud, Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene, Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, Viongozi wa vyama vya siasa na viongozi wa dini.

No comments: