Wednesday, July 27, 2016

ASKARI WA MAUAJI YA MWANDISHI WA HABARI DAUD MWANGOSI AHUKUMIWA JELA MIAKA 15


Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Deo Nsokolo akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya hukumu ya kesi hiyo.
Jinsi mauaji yalivyofanyika.

IRINGA:
MAHAKAMA  kuu ya Tanzania  kanda  ya  Iringa, leo  imemuhukumu kwenda  jela miaka 15 askari wa Kikosi cha  Kutuliza Ghasia (FFU) mwenye  namba G. 2573 Pacificius Cleophace Simon (27)  aliyemuua mwandishi  wa  habari  wa  kituo  cha Chanel Ten, Daudi  Mwangosi.

Akisoma hukumu hiyo, Jaji wa Mahakama hiyo Dkt. Paul Kihwelo alisema kuwa mshtakiwa huyo amekutwa na hatia ya kuua bila kukusudia katika shitaka la pili lililosomwa Mahakamani hapo leo, baada ya la kwanza kusomwa na kukutwa hana hatia.

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa mwezi Februari 12, mwaka 2012 na kufikia hukumu hiyo ya kumtia hatiani na kwamba tukio hilo lilitokea Septemba 2 mwaka 2012 katika kijiji cha Nyololo, wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

No comments: