Saturday, July 23, 2016

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA MJINI DODOMA

  Kundi la Tot Plus likiongozwa na Khadija Kopa akiimba mbele ya Wajumbe wapatao zaidi ya 2000 wa mkutano Mkuu Maalum wa CCM mjini Dodoma leo.
 
Baadhi ya wageni waalikwa kutoka vyama mbalimbali vya upinzani pia walihudhuria mkutano huo wa CCM. Ambapo vyama vya siasa vipatavyo 12 vilialikwa na vyote vimefika katika mkutano huo isipokuwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Wajumbe wapatao zaidi ya 2000 wa mkutano Mkuu maalum wa CCM wakitumbuizwa ndani ya ukumbi wa Dodoma Convetion Center (DCC) ulioko nje kidogo ya mji wa Dodoma, hivi sasa kundi la TOT Plus likiongozwa na Mwana mama mkongwe Khadija Kopa.
 
Baadhi ya Wageni waalikwa wakiwemo mabalozi wa nchi mbalimbali wakiwa ndani ya ukumbi huo leo kwenye mkutano Mkuu maalum wa CCM  mjini Dodoma.
 
Wajumbe wapatao zaidi ya 2000 wa mkutano Mkuu maalum wa CCM wakiwa tayari ndani ya ukumbi wa Dodoma Convetion Center (DCC) kukamilisha mchakato wao wa kumchagua Mwenyekiti mpya wa chama hicho.
 
Baadhi ya Wageni waalikwa kutoka sehemu mbalimbali wakiwa ndani ya ukumbi ambapo leo mkutano Mkuu maalum wa CCM umefanyika kwa ajili ya kumchagua Mwenyekiti mpya wa chama cha Mapinduzi (CCM) kwa miaka kumi, Rais John Pombe Magufuli na kukabidhiwa kijiti hicho kutoka kwa Mwenyekiti ambaye amemaliza muda wake leo, Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete mkutano huo umefanyika ndani ya ukumbi wa Dodoma Convetion Center (DCC) ulioko nje kidogo ya mji wa Dodoma. (Picha zote kwa hisani ya Michuzi blog)

No comments: