Saturday, July 23, 2016

KIKWETE AKABIDHI RASMI UENYEKITI WA CCM KWA DOKTA JOHN MAGUFULI LEO JIONI MKOANI DODOMA

 Mwenyekiti aliyemaliza Muda wake Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na Mwenyekiti mpya wa chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli wakiwapungia mkono Wajumbe wa mkutano Mkuu maalum mara baada ya matokeo kutangazwa rasmi na kwamba Dkt. Magufuli aliibuka mshindi kwa kura zote za ndio 2,398 na hakuna kura iliyoharika.
 
 Mwenyekiti aliyemaliza muda wake leo, Rais wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete akimkabidhi vitendea kazi mbalimbali vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwenyekiti mpya, Rais Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kumaliza kupigiwa kura za ndiyo.
 
 Makamu Mwenyekiti wa Zanzibar Dkt. Shein akimpongeza Mwenyekiti Mpya, Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM. Pichani katikati anayeshuhudia ni Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Dkt. Jakaya Kikwete.
 
  Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrhaman Kinana akimpongeza Mwenyekiti mpya, Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa chama hicho kwa miaka 10.
 
 Mwenyekiti mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mbele ya Wajumbe wa mkutano Mkuu maalum wa chama hicho, mara baada ya kutangazwa rasmi kuwa Mwenyekiti wa CCM.
 
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa akimpongeza Mwenyekiti mpya, Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa chama hicho kwa miaka 10.
 
Mwenyekiti mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akimkumbatia Mwenyekiti mpya, Rais Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kutangazwa rasmi kuwa Mwenyekiti wa chama hicho.
 
 Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano mkuu maalum wa CCM wakipiga kura kumchagua Mwenyekiti mpya wa chama hicho leo mjini Dodoma.
 
 Wajumbe kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini wakipiga kura.
 
 Wajumbe wamekwisha piga kura na maboksi ya kupigia kura yakiwa tayari kuhesabiwa na baadae kutolewa majibu.
 
 Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ally Hassan Mwinyi akipiga kura ya kumchagua Mwenyekiti mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) jioni ya leo.
 
 Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano mkuu maalum wa CCM wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Dodoma Convetion Center,uliopo nje kidogo ya mji wa Dodoma.
 
 Mwenyekiti wa CCM ambaye amemaliza muda wake leo, Rais wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na baadhi ya Wajumbe wa mkutano mkuu, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kabla ya matokeo ya kumpata Mwenyekiti wa chama hicho hayajatangazwa rasmi jioni ya leo.
 
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akijadiliana jambo na Mwenyekiti mstaafu aliyemaliza muda wake leo, Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
 
 Kada Mkongwe wa CCM Mzee Makamba akimpongeza Mpendazoe kwa kurejea CCM.
 







Picha zote kwa hisani ya Michuzi blog mkoani Dodoma.

No comments: