Monday, October 17, 2016

MBINGA WAKUMBUKA MCHANGO WA ALIYEKUWA AFISA ELIMU MSINGI MATHIAS MKALI

Afisa elimu msingi halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, Samwel Komba akizungumza mwishoni mwa wiki wakati wa sherehe ya kumuaga aliyekuwa afisa elimu ya msingi wa wilaya hiyo, Mathias Mkali wa pili kutoka kulia ambaye amehamishiwa mkoa wa Rukwa kuwa afisa elimu taaluma wa mkoa huo. Kushoto ni mgeni rasmi katika sherehe hiyo ambaye ni Meneja wa Kiwanda cha kukoboa kahawa Mbinga, Jonas Mbunda.
Afisa elimu taaluma wa mkoa wa Rukwa, Mathias Mkali kulia akimwonesha  Meneja wa Kiwanda cha kukoboa kahawa Mbinga, Menas Mbunda ambaye alikuwa mgeni rasmi wa sherehe ya kuagwa kwake tuzo maalum iliyotolewa na Rais wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete ya kuipongeza wilaya ya Mbinga kutokana na matokea mazuri katika mitihani ya kumaliza elimu ya msingi darasa la saba kwa miaka miwili 2013/2014 ambapo wilaya hiyo, ilifanya vizuri katika matumizi ya fedha zilizotolewa na serikali kwa ajili ya elimu na kushika nafasi ya kwanza katika mkoa wa Ruvuma.
Afisa elimu taaluma wa mkoa wa Rukwa Mathias Mkali ambaye alikuwa afisa elimu ya msingi katika wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, akizungumza mwishoni mwa wiki wakati wa sherehe ya kumuaga iliyoandaliwa na Wadau mbalimbali wa elimu wilayani humo.
Mgeni rasmi katika sherehe ya kumuaga aliyekuwa Afisa elimu msingi wilaya ya Mbinga ambaye kwa sasa ni Afisa taaluma mkoa wa Rukwa Mathias Mkali, Jonas Mbunda kushoto, akimuongoza Mkali upande wa kulia kukata keki maalum iliyoandaliwa na wadau wa elimu wa wilaya hiyo kutokana na kufurahishwa na mchango mkubwa alioutoa katika suala zima la maendeleo ya elimu wilayani humo.
Baadhi ya wanakamati wa sherehe hiyo wakiwa katika furaha wakati wa zoezi la kutoa zawadi kwa muagwa.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria sherehe fupi ya kumuaga aliyekuwa Afisa elimu msingi wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, Mathias Mkali wakifuatilia matukio katika sherehe hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Uvikambi Mbinga mjini.


No comments: