Saturday, August 5, 2017

RAIS MAGUFULI NA RAIS MUSEVENI WA UGANDA WAWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI KUTOKA HOIMA MPAKA CHONGOLEANI TANGA LEO

Rais Dokta John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mkono na mgeni wake Rais wa Uganda, Yoweri  Kaguta Museveni baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa  mradi mkubwa wa usafirishaji wa mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda mpaka katika bandari ya Tanga, katika sherehe iliyofanyika viwanja vya Chongoleani, mkoani Tanga leo.
Rais Dokta John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda, Yoweri  Kaguta Museveni wakiwasili katika viwanja vya Chongoleani, mkoani Tanga tayari kwa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa  mradi mkubwa wa usafirishaji wa mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda mpaka katika bandari ya Tanga.
Rais Dokta John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais wa Uganda, Yoweri  Kaguta Museveni  wakifurahi jambo na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan wakiwa katika viwanja vya Chongoleani, mkoani Tanga tayari kwa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa  mradi mkubwa wa usafirishaji wa mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda mpaka katika bandari ya Tanga.
Rais Dokta John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais wa Uganda, Yoweri  Kaguta Museveni, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ambaye ni wa tatu kushoto, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa upande wa kulia pamoja na viongozi wengine wakiwa wamesimama wakati wimbo wa taifa ukiimbwa.
Wananchi wakishangilia wakati Rais Dokta John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais wa Uganda, Yoweri  Kaguta Museveni walipowasili katika viwanja vya Chongoleani, mkoani Tanga tayari kwa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa  mradi mkubwa wa usafirishaji wa mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda mpaka katika bandari ya Tanga - Tanzania.              (Picha zote na Ikulu)

No comments: