Tuesday, August 1, 2017

WANANCHI MNAKARIBISHWA KWENYE SHEREHE ZA UWEKAJI JIWE LA MSINGI MRADI WA MAFUTA GHAFI KUTOKA HOIMA NCHINI UGANDA HADI TANGA TANZANIA

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dokta Merdad Kalemani anawaalika wananchi katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi ujenzi wa Bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga, Tanzania.


Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika Agosti 5, 2017 eneo la Chongoleani Jijini Tanga ambapo utahudhuriwa na waasisi wa mradi huo mkubwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni.

No comments: