Saturday, August 5, 2017

RAIS MUSEVENI WA UGANDA AANDALIWA DHIFA YA KITAIFA JIJINI TANGA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wakati wa dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Ikulu ndogo jijini Tanga. Pamoja nao meza kuu ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mama Janeth Magufuli. Hii ikiwa ni bado masaa machache kabla ya uwekaji wa jiwe la Msingi la ujenzi wa mradi mkubwa wa usafirishaji wa Mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda mpaka katika bandari ya Tanga.
 
Sehemu ya mawaziri na manaibu waziri wa Tanzania na Uganda wakiwa wamesimama wakati wa nyimbo za Taifa za nchi hizo mbili na wa Afrika Mashariki kwenye dhifa ya Taifa aliyoiandaa Rais Dokta John Pombe Magufuli kwa heshima ya mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda Ikulu ndogo jijini Tanga Ijumaa usiku.
Sehemu ya viongozi mbalimbali wakiwa wamesimama wakati wa nyimbo za Taifa za nchi hizo mbili na wa Afrika Mashariki kwenye dhifa ya Taifa aliyoandaa Rais Dokta Magufuli kwa heshima ya mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda Ikulu ndogo jijini Tanga Ijumaa usiku.
  Sehemu ya wageni waalikwa wa mataifa mbalimbali wakiwa wamesimama wakati wa nyimbo za Taifa za nchi hizo mbili na wa Afrika Mashariki kwenye dhifa ya Taifa aliyoandaa Rais Dokta Magufuli kwa heshima ya mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda Ikulu ndogo jijini Tanga Ijumaa usiku.
  Wakuu wa Mikoa wakiwa wamesimama wakati wa nyimbo za Taifa za nchi hizo mbili na wa Afrika Mashariki kwenye dhifa ya Taifa aliyoandaa Rais Dpkta Magufuli kwa heshima ya mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda Ikulu ndogo jijini Tanga Ijumaa usiku.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wakizungumza  kwenye dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Ikulu ndogo jijini Tanga, pamoja nao meza kuu ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mama Janeth Magufuli.
 Baadhi ya wasanii wa Kizazi kipywa wakiwa kwenye dhifa ya Taifa aliyoandaa Rais Dokta Magufuli kwa heshima ya mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda Ikulu ndogo jijini Tanga Ijumaa usiku.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni  baada ya dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Ikulu ndogo jijini Tanga. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli akimtambulisha Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kwa  mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni baada ya kumalizika kwa  dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Ikulu ndogo jijini Tanga. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli akimtambulisha Katibu Mkuu wa CCM,  Abdulrahman Kinana  kwa  mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni baada ya kumalizika kwa  dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Ikulu ndogo jijini Tanga. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli akimtambulisha Waziri wa Ardhi, William Lukuvi  kwa  mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni baada ya kumalizika kwa  dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Ikulu ndogo jijini Tanga. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli na  mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wakiagwa kwa saluti na Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama baada ya kumalizika kwa  dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Ikulu ndogo jijini Tanga.  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli akitakiana usiku mwema na  mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni baada ya dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Ikulu ndogo jijini Tanga, pamoja nao ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mama Janeth Magufuli. (Picha na Ikulu)

No comments: