Na Mwandishi wetu,
Dar es Salaam.
JAJI Mkuu, Profesa Ibrahim Juma amezindua kituo cha mafunzo
na habari za Mahakama ili kuwajengea uwezo watumishi.
Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma. |
Akizindua kituo hicho katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
leo Januari 29 mwaka huu, Profesa Juma alisema malengo ya kufanya hivyo ni kuhakikisha
haki inawafikia wananchi kwa wakati na kwa urahisi zaidi.
Profesa Juma alisema kituo hicho kimejengwa kwa kushirikiana
na Benki ya Dunia.
Jaji Mkuu alifafanua kuwa wanawajengea uwezo watumishi wa
Mahakama kwa sababu kuna mambo mengine hawakusoma wakiwa chuoni.
Alisema kuwa Tehama inarahisisha kazi kwa kutoa haki kwa
wakati na kwa urahisi, pia kuwafikia wananchi.
Maeneo mapya yanayotakiwa kufanyiwa kazi na watumishi wa
Mahakama alieleza kuwa ni makosa ya mtandao, yanayotokana na miamala ya simu na
dawa za kulevya.
Jaji Mkuu, Profesa Juma alisema Mahakimu na waendesha
mashtaka wakipata mafunzo watakuwa na uelewa mmoja katika kutoa haki.
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bella Bird akizungumzia
mfumo huo wa Tehama alisema utasaidia kuwafikia wananchi wengi kwa urahisi na
watapata haki kwa wakati.
No comments:
Post a Comment