Na Mwandishi wetu,
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dokta John Pombe Magufuli ameitaka idara ya Uhamiaji hapa nchini kuendelea
kushughulikia wahamiaji haramu pasipo kumwogopa mtu yeyote yule.
Dokta Magufuli alitoa agizo hilo leo
wakati alipokuwa akizungumza kwenye uzinduzi wa hati ya kusafiria ya
Kielektroniki jijini Dar es Salaam, huku akiipongeza Wizara ya mambo ya ndani
kwa utendaji mzuri wa kazi.
Alisema kuwa Wizara hiyo anaipongeza
kwa sababu Waziri mwenye dhamana na Wizara hiyo wakati anamteua alimpeleka pale
akimwambia kwamba kuna changamoto nyingi na kwa kiasi kikubwa sasa zimetatuliwa.
“Na ndio maana Kamishna wa imagration
alivyoniambia kuwa wanahitaji nyumba za wafanyakazi kule Dodoma sijatoa
kwa taasisi nyingine nyumba, lakini nilitoa hela Serikalini tukatoa nyumba
103 kule Dodoma ni kwasababu ya uzalendo ambao nimeanza kuuona,
“Lakini pia mimi nimejiandaa kuja
kutoa hela nyingine makao makuu mmeshakubali kuhamia Dodoma na hapa palivyokaa
kaa hapa hapakai kama makao makuu ya imagration, ninajua kuna baadhi ya
wafanyakazi watalaumu kuhamia Dodoma”, alisema.
Alisema kuwa atawapatia bilioni 10
wakati wowote kuanzia sasa ili waweze kuanza kazi ya ujenzi wa Ofisi za makao
makuu ya Uhamiaji Dodoma.
“Ni lazima tuwe na jingo zuri katafuteni eneo nitawapa bilioni 10
wakati wowote mtakapozihitaji muanze kujenga makao makuu na ninatoa hivi kwa
shukurani mnayofanya kwa utendaji wenu mzuri wa kazi endeleeni kuchapa kazi na
kushughulikia wahamiaji haramu bila kumuogopa mtu yeyote”, alisema Dokta Magufuli.
No comments:
Post a Comment