Ummy Mwalimu. |
SERIKALI hapa nchini kupitia Wizara
yake ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa tahadhari
kuhusu ugonjwa wa Chikungunya ambao umeripotiwa na vyombo vya habari
kutokea Mombasa nchini Kenya.
Waziri wa Wizara hiyo, Ummy Mwalimu
ametoa taarifa yake leo Januari 19 mwaka huu akisema kuwa mpaka sasa Shirika la
Afya Duniani (WHO) bado halijatoa taarifa rasmi lakini Serikali hapa nchini inatoa
tahadhari kuzingatia muingiliano mkubwa wa watu baina ya nchi hizi mbili Kenya
na Tanzania.
Kwa ujumla Wizara ya afya imefafanua
kuwa ugonjwa wa Chikungunya unasababishwa na kirusi ambacho kinaenezwa na mbu aina
ya Aedes na kusema ugonjwa huo si mgeni nchini Tanzania kwani ulishawahi
kutokea.
Taarifa zaidi hii hapa;
No comments:
Post a Comment