Na Mwandishi wetu,
DENI la zaidi ya shilingi milioni 800 ambalo lilikuwa likidaiwa na wakulima wa Korosho kwa msimu wa mwaka 2016/2017 kwa vyama vya ushirika (AMCOS) Mkoa wa Mtwara hatimaye limelipwa.
Mwenyekiti wa bodi ya chama kikuu cha ushirika cha Masasi, Mtwara Cooperative Union (MAMCU) Joseph Kidando alisema kuwa tayari kiasi hicho cha fedha kimeingizwa katika akaunti za vyama vya msingi kwa ajili ya kugawanywa kwa wakulima.
Aidha Mwenyekiti huyo alifafanua kuwa wamelazimika kulipa deni hilo kutokana na wao kuwa walezi wa AMCOS na wakulima kwa ujumla na ametaja sababu za kuchelewesha kulipwa kwa fedha hizo ni upotevu wa fedha uliosababishwa na makosa ya viongozi wa AMCOS husika.
Kwa upande mwingine Kidando ameeleza kuwa sababu nyingine kubwa iliyosababisha upotevu wa fedha hizo ni kuingizwa kimakosa katika akaunti tofauti za vyama vya msingi, ambapo baadhi ya viongozi wasiokuwa waaminifu waliamua kuzifanyia matumizi yao binafsi.
No comments:
Post a Comment