Na Muhidin Amri,
Tunduru.
WANAFUNZI wanaosoma kidato cha tano
na sita katika shule ya Sekondari Nandembo kata ya Nandembo Halmashauri Wilaya
ya Tunduru Mkoani Ruvuma, hivi sasa wataweza kuondokana na kero ya mahali pa
kulala baada ya kukamilika kwa ujenzi wa mabweni mawili yenye uwezo wa kulaza
wanafunzi 160 kwa wakati mmoja.
Mary Ndunguru ambaye ni Mkuu wa shule
hiyo alisema kuwa ujenzi wa mabweni hayo hadi kukamilika kwake zimetumika
shilingi milioni 150 kwa kutumia mfumo wa Force Account ambapo mafundi wadogo
ndiyo wanaotumika kufanya kazi hiyo badala ya kutumia Wakandarasi wakubwa.
Alisema kuwa ili kuweza kutosheleza
mahitaji husika kila bweni litatumiwa na watoto 50 lakini baada ya bweni moja
kuungua moto mwaka jana hivi sasa wanabweni moja tu na wanafunzi wengine
hulazimika kuishi kwenye hosteli za Kanisa Katoliki Nandembo kwa gharama za
wazazi wao.
Ndunguru alifafanua kuwa bado shule
ina uhitaji mkubwa wa mabweni kwani hata yale yanayotarajia kukamilika ujenzi
wake yamejengwa kwa ajili ya matumizi ya kidato cha tano na sita, hivyo kuiomba
Serikali iangalie uwezekano wa kujenga mabweni mengi zaidi yatakayoweza kulaza wanafunzi
wa kidato cha kwanza hadi nne nao waweze kuishi katika mazingira ya shule.
“Tunaiomba Serikali yetu iangalie
uwezekano wa kutujengea mabweni haya, maabara na ukumbi wa chakula shule hii ni
ya bweni lakini bado tunakabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa miundombinu
yake”, alisema Ndunguru.
No comments:
Post a Comment