Na Mwandishi wetu,
BAADHI ya Wananchi ambao wamejiunga
na mfuko wa Bima ya afya katika Halmashauri ya Busokelo Wilayani Rungwe Mkoa wa
Mbeya wamelalamikia wauguzi kwenye vituo vya afya katika halmashauri hiyo,
kuwabagua wagojwa wanaokwenda kutibiwa wakiwa na kadi za bima ya afya na kutoa
kipaumbele kwa wagonjwa wanaolipa fedha taslimu hali ambayo wamedai kuwa
inakwamisha jitihada za Serikali kuhamasisha wananchi kujiunga na bima za fya
nchini.
Wananchi hao wametoa malalamiko yao
mbele ya Mbunge wa jimbo la Busokelo, Atupele Fred Mwakibete wakati walipokuwa kwenye
mkutano wa hadhara baada ya Mbunge huyo kufika katika kijiji cha Matamba kwa
lengo la kukagua ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho.
Akizungumza na wananchi hao, Mwakibete
ameahidi kuyafanyia kazi malalamiko hayo huku akiwahimiza wananchi hao kuungana
pamoja kukamilisha ujenzi wa jengo la kisasa la zahanati hiyo ambalo kutokana
na ubora wake linaweza kubadilishwa na kuwa kituo cha afya.
Katika risala yao wananchi hao
wamedai kuwa mbali na ujenzi wa zahanati hiyo pia wanamipango ya ujenzi wa
nyumba mbili za wauguzi hivyo wakaiomba Serikali pamoja na wadau wengine
kuwaunga mkono.
No comments:
Post a Comment