Na Muhidin Amri,
Madaba.
WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA) Mkoani
Ruvuma, ametakiwa kumaliza ujenzi wa majengo ya Ofisi za Halmashauri ya Wilaya
ya Madaba Mkoani humo kwa wakati uliopangwa, ili kuweza kuwafanya watumishi
waweze kupata sehemu nzuri ya kufanya kazi zao pale wanapowahudumia wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christine Mndeme. |
TBA wameonywa pia wasitumie muda
mwingi kukaa Ofisini badala ya kufanya kazi husika.
Palolet Mgema ambaye ni Mkuu wa
Wilaya ya Songea alisema hayo juzi wakati alipokuwa amefanya ziara yake ya
kushitukiza, kwa lengo la kukagua ujenzi huo.
Kadhalika Mkuu huyo wa Wilaya
alisikitishwa kazi ya ujenzi ikiwa inasuasua huku kukiwa na idadi ndogo ya
vibarua na mafundi.
Alisema kuwa kwa mujibu wa
makubaliano ya mkataba husika wa kazi hiyo ilitakiwa hivi sasa ifikie hatua ya
kusimamisha nguzo, lakini kutokana na kasi ndogo ya ujenzi hali hiyo imekuwa
kinyume na badala yake wamefikia hatua ya kuchimba mashimbo huku wakiwa nyuma
ya mkataba kwa miezi mitano.
“Kwa kweli lazima niseme kweli hawa
wenzetu wa TBA wanatuangusha, licha ya kuwa ni taasisi ya Serikali lakini utendaji
wao wa kazi haujanifurahisha hata kidogo, wanatakiwa wahakikishe wanaongeza
nguvu kazi katika mradi huu ili watumishi wetu waweze kupata ofisi za
kuwahudumia wananchi”, alisema Mgema.
Serikali imetenga jumla ya shilingi
bilioni 1.1 kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
ya Wilaya ya Madaba ambapo kati ya fedha hizo shilingi milioni 500 na shilingi
milioni 600 zimetolewa mwezi Desemba mwaka jana, ambapo hata hivyo bado Wakala
huyo wa majengo anaonekana kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa wakati.
Kwa upande wake mwakilishi kutoka TBA
ambaye ni msimamizi wa mradi huo, Ngwilimi Magese alikiri kuwa nyuma ya kazi huku
akijitetea kwamba tatizo lililowafanya wachelewe ni kutokana na ukosefu wa maji
na umeme.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
Wilaya ya Madaba, Shafi Mpenda kwa upande wake alimshukuru Rais Dokta John
Magufuli kwa kutoa fedha za ujenzi wa mradi huo huku akisikitishwa na kasi
ndogo ya utendaji kazi wa Wakala huyo.
Alisema kuwa kwa mujibu wa mkataba wa
mradi huo inatakiwa kila mwezi wakae kikao kimoja (Site meeting) lakini
haifanyiki hivyo badala yake tangu walipokaa mwezi Novemba mwaka jana,
hawajakaa tena na kila anapowakumbusha TBA kwa ajili ya kufanya hivyo wamekuwa
wakikwepa kutekeleza jambo hilo.
No comments:
Post a Comment