MAMIA ya waombolezaji wamejitokeza
kuaga mwili wa Alfred Nzigilwa, ambaye ni baba mzazi wa Askofu Msaidizi wa
Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa katika ibada
iliyofanyika Parokia ya Roho Mtakatifu Segerea.
Mzee Nzigilwa (87) alifariki dunia
Desemba 29,2017 nyumbani kwake Tabata Chang'ombe jijini Dar es Salaam.
Imeelezwa alikuwa akipata matibabu
mara kwa mara katika hospitali za Muhimbili, Madonna na Regency kutokana na
maradhi ya tumbo na moyo kutanuka.
Viongozi kadhaa wamemuelezea mzee
Nzigilwa wakisema alikuwa mmoja wa viongozi mahiri wa kanisa kwa muda mrefu na
alikuwa msaada katika usuluhishi wa migogoro ya ndoa.
Padri Stephano Kaombe amesema msiba
huo umekuwa na sura ya kijimbo kwa sababu ya nafasi ya Askofu Nzigilwa lakini
pia kwa maisha aliyoishi mzee huyo.
Mazishi yamefanyika leo Jumatatu
Januari Mosi, 2018 katika makaburi yaliyopo Pugu jijini Dar es Salaam.
Mwananchi.
No comments:
Post a Comment