MABINGWA watetezi wa ligi kuu
Tanzania Bara Yanga, leo wamesaini mkataba wa miaka mitatu na kampuni ya
utengenezaji wa vifaa vya michezo, Macron wenye thamani ya shilingi bilioni
mbili.
Katika mkataba huo uliosainiwa kwenye
makao makuu ya klabu hiyo, Yanga itatoa haki zote za utengenezaji na usambazaji
wa jezi zao huku pia nembo ya kampuni ya Macron, itaanza kuonekana kwenye jezi
za Yanga SC.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Yanga,
Charles Mkwasa amewaonya wote wanaouza jezi za klabu hiyo bila kuwepo kwa
makubaliano watawachukulia hatua za kisheria kwa sababu sasa yupo mwenye haki
ya kufanya hivyo.
Pia Mkwasa amewakaribisha wawekezaji
zaidi ndani ya klabu hiyo.
Naye Mkurugenezi Mtendaji wa kampuni
hiyo hapa Tanzania, Suleiman Karim amewahakikishia wanayanga kuwa klabu hiyo
itapata faida kupitia mauzo ya jezi orijino za klabu.
Kampuni ya Macron inafanya kazi katika
nchi zaidi ya 16 duniani ikiwemo England, Italia na Ufaransa.
Hivi karibuni kampuni hiyo iliingia
mkatata wa miaka 2 na timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) wenye thamani ya shilingi
milion 800.
No comments:
Post a Comment