Pierre Lechantre. |
KLABU ya Simba leo imemtangaza rasmi
Mfaransa Pierre Lechantre, kuwa Kocha mpya atakayekinoa kikosi hicho, ambacho
kilikuwa hakina mwalimu baada ya kumfukuza aliyekuwa kocha wake, Joseph Omog
mwishoni mwa mwaka jana.
Taarifa hiyo iliyotolewa na Msemaji
Mkuu wa Klabu hiyo, Haji Manara imeeleza kuwa kocha huyo ataanza kazi mara moja
na atasaidiwa na kocha msaidizi wa sasa Masoud Djuma.
Masoud ambaye alikuwa akikaimu nafasi
hiyo, na kwamba Mfaransa huyo atashuhudia mchezo wa Simba SC dhidi ya Singida
United leo Januari 18 mwaka huu katika uwanja wa Taifa.
Mfaransa huyo alishawahi kukinoa
kikosi cha timu ya taifa ya Cameroun kilichoshinda ubingwa wa Afrika mwaka 2000
na ameshawahi kushinda tuzo ya kocha bora wa bara la Afrika 2001.
Soma zaidi taarifa hiyo kutoka Simba
SC;
TAARIFA KWA UMMA
Klabu ya Simba inayofuraha kubwa
kuwajulisha Wanachama na washabiki wake kwamba imempata kocha wake mkuu mpya, Mfaransa
Pierre Lechantre.
Kocha huyo mzoefu ataanza kazi mara
moja na atasaidiwa na kocha msaidizi wa sasa Masoud Djuma ambaye alikuwa
akikaimu nafasi hiyo.
Kocha Lichantre keshawahi kufundisha
vilabu kadhaa duniani kikiwemo kikosi cha timu ya Taifa ya Cameroun kilichotwaa
ubingwa wa Africa 2000.
Kocha huyo pia alipata kuwa kocha
bora wa Afrika mwaka 2001 na pia barani Asia mwaka 2012.
Lechantre amekuja pia na kocha wa
viungo Mmorocco Mohammed Aymen Hbibi, na leo jioni kocha Lechantre ataishuhudia
Simba ikicheza na Singida United kwenye Uwanja wa Taifa.
No comments:
Post a Comment