Na Muhidin Amri,
Songea.
MBUNGE wa Viti maalum Mkoa wa Ruvuma,
Sikuzan Chikambo amewataka wanawake wa mkoa huo kujituma na kufanya kazi kwa
bidii ili waweze kujiletea maendeleo katika familia zao na kuweza kuondokana na
umaskini.
Aidha Chikambo amewakumbusha wanawake
hao kutumia fedha wanazopata kuanzisha vikundi vya ujasiriamali na kutumia kwa
ajili ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa nyumba bora za kuishi na kupeleka watoto
wao shule.
Mbunge huyo alitoa wito huo mwishoni
mwa wiki wakati akizungumza na wanachama wa Jumuiya ya Wanawake ya Chama
cha Mapinduzi (UWT) Wilaya ya Songea Mkoani hapa na kusisitiza kuwa wanawake
hao wanao mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi.
Chikambo alikuwa mjini hapa kwa ajili
ya kushiriki kampeni za kumnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Songea mjini
kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dokta Damas Ndumbaro ambaye
amechaguliwa na kushinda kwa kura nyingi.
Hata hivyo aliwataka kuongeza juhudi
kwa kufanya kazi na kujiunga katika vikundi hivyo sambamba na kutengeneza
bidhaa zenye ubora ambao unakubalika katika viwango vya kimataifa ili waweze kuwa
na uhakika wa kupata soko zuri la kuuza bidhaa zao.
No comments:
Post a Comment