Sunday, March 1, 2015

KAMATI KUU YAPOKEA KIFO CHA KOMBA KWA MASIKITIKO

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati Kuu.


Na Mwandishi maalum,
Dar.

KAMATI Kuu ya CCM imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kusikitisha za kifo cha Mjumbe wa halmashauri kuu wa miaka mingi, msanii wa Chama Cha Mapinduzi, kada mzoefu Kapteni John Komba.

Kwa maneno ya Mwenyekiti wa chama hicho, alisema kifo cha Komba ni pengo lisilozibika na Chama Cha Mapinduzi kimepata pigo kubwa, huku Komba akibaki kwenye historia iliyotukuka.

Wasimamishwa:

Pia Kamati kuu imewasimamisha, Profesa Anna Tibaijuka ambaye ni mjumbe wa Kamati kuu, Andrew Chenge ambaye ni  mjumbe wa Halmashauri kuu pamoja na William Ngeleja mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kuhudhuria vikao vya maamuzi vya chama kwa kipindi ambacho kamati hii ndogo ya maadili wakiendelea na kazi yao ya kupitia baadhi ya nyaraka mbalimbali zinazohusiana na suala hili. 

Akizungumzia kuhusu adhabu walizopewa wale wanachama sita, waliojitokeza na kuanza shughuli za kampeni za kuwania nafasi ya kuchaguliwa na chama kugombea urais alisema kamati ndogo ya maadili inaendelea na uchunguzi wake.

No comments: