Saturday, February 28, 2015

BREAKING NEWS: KAPTENI JOHN KOMBA MBUNGE WA MBINGA MAGHARIBI AFARIKI DUNIA

Kapteni Komba, akiwajibika jukwaani kwenye bendi ya TOT enzi ya uhai wake.


Na Mwandishi wetu,
Dar.

TAARIFA za uhakika zilizotufikia hivi punde, kutoka kwenye chumba chetu cha habari zinaeleza kuwa, aliyekuwa Mkurugenzi wa Tanzania One Theater (TOT) na Mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi mkoani Ruvuma, Kapteni John Komba (pichani) amefariki dunia.

Kapteni Komba amefariki dunia jioni hii, katika Hospitali ya TMJ Mikocheni Jijini Dar es Salaam, ambako alikuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Mtoto wake, Jerry Komba amesema chanzo cha kifo cha baba yake ni kushuka kwa sukari akiwa nyumbani kwake Mbezi, ambapo baada ya kukumbwa na tatizo hilo walimpeleka katika hospitali hiyo, kwa ajili ya matibabu zaidi na ambako mauti yalimkuta.


Mwandishi wetu, kwa kushirikiana na vyanzo mbalimbali vya habari ameelezwa kuwa taratibu za kuhamisha mwili wa marehemu, kuupelea katika hospitali ya Lugalo zinaendelea kufanyika.

Mtandao huu utaendelea kukupatia taarifa zaidi, juu ya kifo cha Mbunge huyo wa Mbinga Magharibi, zaidi hapo baadae.

Gwiji la Matukio Ruvuma, tunaungana na familia ya marehemu, wana TOT pamoja na  Watanzania wote kuombeleza kifo cha Kapteni Komba.

Mungu awatie nguvu na faraja, ndugu na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu na chenye majonzi mazito.

Bwana ametoa na Bwana alitwaa, jina lake lihimidiwe………………………….. Amen.


No comments: