Saturday, February 14, 2015

WAKULIMA KUNUFAIKA NA MICHE YA MIKOROSHO


Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Chande Nalicho akipokea miche ya mikorosho bora kutoka kwa Mwenyekiti wa mfuko wa kuendeleza zao la korosho Tanzania, Athuman Nkinde. (kushoto)


Mkuu wa wilaya ya Tunduru Chande Nalicho, akimkabidhi miche ya mikorosho kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Chiza Marando wa upande wa kulia kwa ajili ya kuisambaza kwa wakulima.
Na Steven Augustino,
Namtumbo.

Halmashauri ya  wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma, imepongeza juhudi za  Mfuko wa Kuendeleza zao la Korosho Tanzania (WAKFU) kwa kuwapatia mgao wa mikorosho mipya, ikiwa ni juhudi ya serikali kuinua kipato kwa wananchi wake na kuendeleza kilimo cha zao hilo.

Hayo yalisemwa na wawakilishi wa halmashauri hiyo, akiwemo kaimu afisa kilimo wa wilaya hiyo, Aniseth Ndunguru na mratibu wa zao hilo Joseph Ngatunga wakati wakikabidhiwa miche mipya 10,000 ya korosho.

Aidha viongozi hao kwa niaba ya halmashauri hiyo, pamoja na pongezi hizo pia walimhakikishia Mwenyekiti wa mfuko wa kuendeleza zao hilo Tanzania, Athuman Nkinde kwamba, wapoimara katika kuwawezesha wakulima kielimu juu ya kilimo cha zao hilo, pamoja na kuisambaza kwa wingi kwa wakulima wao.

Walisema katika kipindi cha msimu wa kilimo mwaka 2014, halmashauri ilipokea miche bora 10,000 yenye thamani ya shilingi milioni 55 ambayo iliyotolewa na mfuko huo.


Akifafanua mbele ya Mwenyekiti wa mfuko huo, Ngatunga alisema kuwa kiasi cha mikorosho ambayo wamegawiwa wakulima kwa msimu huu, pia imepangwa kusambazwa tena kwa wakulima waliopo kata za Ligela, Mchomoro, Limamu na Likuyuseka.

Awali akimkabidhi miche ya mikorosho hiyo, Mwenyekiti huyo wa WAKFU Athuman Nkinde alieleza mfuko huo, umedhamiria kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya kilimo kwanza.

Alisema mikorosho hiyo inatakiwa kusambazwa na kugawiwa bure kwa wakulima wote nchini, kutokana na tayari mfuko kugharimia gharama zote za uendeshaji juu ya zoezi hilo.

Miche hiyo husambazwa kwa wakulima baada ya kufanyiwa usanifu na Wataalamu wa mimea, kutoka kituo cha utafiti cha Naliendele ambacho kimeweka matawi yake katika wilaya ya Tunduru, kinacho hudumia kanda ya kusini, Mpwapwa kinachohudumia wakulima kanda ya ziwa na Mkuranga kinahudumia wakulima wa kanda ya Mashariki na Kaskazini.

Aliendelea kueleza kuwa sambamba na ongezeko la uzalishaji huo, pia mfuko umeandaa utaratibu wa kugawa mashine maalumu kwa ajili ya kuwasaidia

No comments: