Tuesday, February 24, 2015

CRDB YAIKOPESHA SERIKALI BILIONI 15 KULIPA MADENI YA WAKULIMA



Na Mwandishi wetu,
Iringa.

SERIKALI imepata mkopo wa Sh. bilioni 15 kulipa madeni ya mazao ya nafaka ambayo wakulima wanaidai kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA).

Waziri Mkuu,  Mizengo Pinda, alisema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Iringa akiwa kwenye ziara ya kikazi ya kukagua maendeleo mkoani humo.

Akizungumza baada ya kukagua Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo (SACCOS) cha Mazombe, kilichopo Ilula, wilaya ya Kilolo, mwishoni mwa wiki iliyopita, Pinda alisema katika kipindi cha mwezi huu, serikali imepata mkopo huo kutoka Benki ya CRDB na kusambazwa kwenye mikoa mbalimbali ili kuwalipa wakulima hao.

Alisema hadi kufikia Machi, mwaka huu, serikali itahakikisha inamaliza kulipa madeni kwa wakulima waliouza mazao yao kwa NFRA.

No comments: