Sunday, February 22, 2015

AKATWA SEHEMU ZA SIRI HUKU ZIKIACHWA ZINABEMBEA



Na Amon Mtega,
Tunduru.

MKAZI mmoja wa kijiji cha Majimaji, wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Patrick Vitus (70) amekatwa sehemu zake za siri na kuziacha zikiwa zinabembea na mtu aliyefahamika kwa jina la Zainabu Said (32) ambaye anadaiwa kuwa ni mpwa wake, baada ya kumkatalia kwenda kumfuata mme wa Zainabu aliyekuwa kwa mke mdogo.

Akizungumza na kwa njia ya simu Afisa mtendaji wa kijiji hicho, Hussein Mkali alisema kuwa tukio hilo lilitokea February 20 mwaka huu majira ya usiku katika maeneo ya mashamba ya kijiji hicho, ambako walikuwa wakifanya shughuli za kilimo.

Mkali alisema kuwa Vitus alikatwa nyeti hizo na kuziacha zikiwa zinabembea baada ya kumkatalia Zainabu, kumpeleka kwa mme wake ambaye alidaiwa kuwa alikuwa kwa mke mdogo ambaye ni mke wake. 


Alifafanua kuwa mme wa Zaibu Said ni Mussa Said (40) ambaye ndiye aliyeenda kulala kwa mke mwingine, ambaye jina lake halikupatikana mara moja  na kumsababishia Patrick Vitus kukatwa sehemu zake za siri na kumfanya apatwe na jeraha hilo ambalo humsababishia maumivu makali. 

Baada ya kutokea kwa tukio hilo, ofisi ya kijiji imemkamata Zainabu na kumpeleka katika kituo cha polisi mjini Tunduru, ambako ndiko maelezo zaidi ya kuhusiana na tukio hilo yatatolewa huku mjeruhiwa akiwa amepelekwa Hospital ya Tunduru.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikhela kupitia afisa habari wake wa mkoa alisema, taarifa za tukio hilo katika kituo cha polisi cha Tunduru mjini, zimefika na muda wowote taarifa rasmi zitatolewa.


No comments: