Wednesday, February 18, 2015

UTEUZI WA WAKUU WA WILAYA WAPYA NA WALE WANAOBAKIA KATIKA VITUO VYAO VYA KAZI HUU HAPA



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU
Anuani ya Simu: WAZIRI MKUU
Simu Nambari: 026 2322904
e-mail: pm@pmo.go.tz
S.L.P 980
DODOMA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI:

Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya ili kuboresha utendaji kazi. Mabadiliko hayo yamezingatia kuwepo kwa nafasi wazi ishirini na saba (27) zilizotokana na:

a) Kufariki dunia Wakuu wa Wilaya 3;
b) Kupandishwa cheo Wakuu wa Wilaya 5 kuwa Wakuu wa Mikoa;
c) Kupangiwa majukumu mengine Wakuu wa Wilaya 7; na
d) Kutengua uteuzi wa Wakuu wa Wilaya 12.

Katika mabadiliko hayo, Mheshimiwa Rais amewateua Wakuu wapya wa Wilaya 27 ili kujaza nafasi hizo wazi.
Aidha, Wakuu wa Wilaya sitini na nne (64) wamebadilishwa vituo vya kazi na Wakuu wa Wilaya arobaini na mbili (42) wameendelea kubaki katika vituo vya sasa.

1) Wakuu wa Wilaya waliofariki dunia

JINA NA WILAYA

1. Capt. (mst) James C. Yamungu Serengeti
2. Anna J. Magoha Urambo
3 Moshi M. Chang’a Kalambo

2) Wakuu wa Wilaya waliopandishwa cheo

Wakuu wa Wilaya wafuatao wamepandishwa cheo kuwa Wakuu
wa Mikoa

JINA WILAYA MKOA ALIOPANGIWA

1. John Vianney Mongela Arusha Kagera
2. Amina Juma Masenza Ilemela Iringa
3. Dkt. Ibrahim Hamis Msengi Moshi Katavi
4. Halima Omari Dendego Tanga Mtwara
5. Daudi Felix Ntibenda Karatu Arusha

3) Wakuu wa Wilaya waliopangiwa majukumu mengine

Wakuu wa Wilaya ambao uteuzi wao umetenguliwa na
watapangiwa kazi nyingine ni hawa wafuatao;

JINA NA WILAYA

1. Brig. General Cosmas Kayombo Simanjiro
2. Col. Ngemela Elson Lubinga Mlele
3. Juma Solomon Madaha Ludewa
4. Mercy Emanuel Silla Mkuranga
5. Ahmed Ramadhan Kipozi Bagamoyo
6. Mrisho Gambo Korogwe
7. Elinas Anael Pallangyo Rombo

4) Wakuu wa Wilaya Wanaotenguliwa

Wakuu wa Wilaya ambao uteuzi wao umetenguliwa kutokana na
sababu za umri, kiafya na nyinginezo na vituo vyao ni kama
inavyoonekana hapa chini:

JINA NA WILAYA

1. James Kisota Ole Millya Longido
2. Elias Wawa Lali Ngorongoro
3. Alfred Ernest Msovella Kongwa
4. Dany Beatus Makanga Kasulu
5. Fatma Losindilo Kimario Kisarawe
6. Elibariki Emanuel Kingu Igunga
7. Dr. Leticia Moses Warioba Iringa
8. Evarista Njilokiro Kalalu Mufindi
9. Abihudi Msimedi Saideya Momba
10. Martha Jachi Umbula Kiteto
11. Khalid Juma Mandia Babati
12. Eliasi Goroi Boe Boe Goroi Rorya

5) Wakuu wa Wilaya wapya walioteuliwa

Wakuu wa Wilaya wapya walioteuliwa na Wilaya zao ni
wafuatao;

JINA JINSI NA WILAYA

1. Mariam Ramadhani Mtima KE Ruangwa
2. Dkt. Jasmine B. Tiisike KE Mpwapwa
3. Pololeti Mgema ME Nachingwea

JINA JINSI NA WILAYA

4. Fadhili Nkurlu ME Misenyi
5. Felix Jackson Lyaniva ME Rorya
6. Fredrick Wilfred Mwakalebela ME Wanging’ombe
7. Zainab Rajab Mbussi KE Rungwe
8. Francis K. Mwonga ME Bahi
9. Col. Kimiang’ombe Samwel Nzoka ME Kiteto
10. Husna Rajab Msangi KE Handeni
11. Emmanuel Jumanne Uhaula ME Tandahimba
12. Mboni Mhita KE Mufindi
13. Hashim S. Mngandilwa ME Ngorongoro
14. Mariam M. Juma KE Lushoto
15. Thea Medard Ntara KE Kyela
16. Ahmad H. Nammohe ME Mbozi
17. Shaban Kissu ME Kondoa
18. Zelote Stephen ME Musoma
19. Pili Moshi KE Kwimba
20. Mahmoud A. Kambona ME Simanjiro
21. Glorius Bernard Luoga ME Tarime
22. Zainab R. Telack KE Sengerema
23. Bernard Nduta ME Masasi
24. Zuhura Mustafa Ally KE Uyui
25. Paulo Makonda ME Kinondoni

JINA JINSI NA WILAYA

26. Mwajuma Nyiruka KE Misungwi
27. Maftah Ally Mohamed ME Serengeti

6) Wakuu wa Wilaya waliobadilishwa Vituo

Wakuu wa Wilaya wafuatao wamebadilishwa vituo vya kazi
kama ifuatavyo;

JINA JINSIA NA WILAYA ATOKAYO AENDAYO

1. Nyerembe Deusdedit Munasa ME Arumeru Mbeya
2. Jordan Mungire Obadia Rugimbana ME Kinondoni Morogoro
3. Fatma Salum Ally KE Chamwino Mtwara
4. Lephy Benjamini Gembe ME Dodoma Mjini Kilombero
5. Christopher Ryoba Kangoye ME Mpwapwa Arusha
6. Omar Shaban Kwaang’ ME Kondoa Karatu
7. Francis Isack Mtinga ME Chemba Muleba
8. Elizabeth Chalamila Mkwasa KE Bahi Dodoma
9. Agnes Elias Hokororo (Mb) KE Ruangwa Namtumbo
10. Regina Reginald Chonjo KE Nachingwea Pangani
11. Husna Mwilima KE Mbogwe Arumeru
12. Gerald John Guninita ME Kilolo Kasulu
13. Bi Zipporah Lyon Pangani KE Bukoba Igunga
14. Col. Issa Suleimani Njiku ME Missenyi Mlel
16. Bw. Richard Mbeho ME Biharamulo Momba
17. Bw. Lembris Marangushi Kipuyo ME Muleba Rombo
18. Ramadhani Athuman Maneno ME Kigoma Chemba
19. Venance Methusalah Mwamoto ME Kibondo Kaliua
20. Gishuli Mbegesi Charles ME Buhigwe Ikungi
21. Novatus Makunga ME Hai Moshi
21. Anatory Kisazi Choya ME Mbulu Ludewa
22. Christine Solomoni Mndeme KE Hanang’ Ulanga
23. Jackson William Musome ME Musoma Bukoba
24. John Benedict Henjewele ME Tarime Kilosa
25. Dkt. Norman Adamson Sigalla ME Mbeya Songea
26. Dr. Michael Yunia Kadeghe ME Mbozi Mbulu
27. Crispin Theobald Meela ME Rungwe Babati
28. Magreth Ester Malenga KE Kyela Nyasa
29. Said Ali Amanzi ME Morogoro Singida
30. Antony John Mtaka ME Mvomero Hai
31. Elias Choro John Tarimo ME Kilosa Biharamulo
32. Francis Cryspin Miti ME Ulanga Hanang’
33. Hassan Elias Masala ME Kilombero Kibondo
34. Angelina Lubalo Mabula KE Butiama Iringa
35. Farida Salum Mgomi KE Masasi Chamwino
36. Wilman Kapenjama Ndile ME Mtwara Kalambo
37. Ponsian Damiano Nyami ME Tandahimba Bariadi
38. Mariam Sefu Lugaila KE Misungwi Mbogwe
39. Mary Tesha Onesmo KE Ukerewe Buhigwe
40. Karen Kemilembe Yunus KE Sengerema Magu
41. Josephine Rabby Matiro KE Makete Shinyanga
42. Joseph Joseph Mkirikiti ME Songea Ukerewe
43. Abdula Suleiman Lutavi ME Namtumbo Tanga
44. Ernest Ng’wenda Kahindi ME Nyasa Longido
45. Anna Rose Ndayishima Nyamubi KE Shinyanga Butiama
46. Rosemary Kashindi Kirigini (Mb) KE Meatu Maswa
47. Abdallah Ali Kihato ME Maswa Mkuranga
48. Erasto Yohana Sima ME Bariadi Meatu
49. Queen Mwanshinga Mulozi KE Singida Urambo
50. Yahya Esmail Nawanda ME Iramba Lindi
51. Manju Salum Msambya ME Ikungi Ilemela
52. Saveli Mangasane Maketta ME Kaliua Kigoma
53. Bituni Abdulrahman Msangi KE Nzega Kongwa
54. Lucy Thomas Mayenga KE Uyui Iramba
55. Majid Hemed Mwanga ME Lushoto Bagamoyo
56. Muhingo Rweyemamu ME Handeni Makete
57. Hafsa Mahinya Mtasiwa KE Pangani Korogwe
58. Dr. Nasoro Ali Hamidi ME Lindi Mafia
59. Festo Shemu Kiswaga ME Nanyumbu Mvomero
60. Sauda Salum Mtondoo KE Mafia Nanyumbu
61. Seleman Mzee Seleman ME Kwimba Kilolo
62. Esterina Julio Kilasi KE Wanging’ombe Muheza
63. Subira Hamis Mgalu KE Muheza Kisarawe
64. Jacqueline Jonathan Liana KE Magu Nzega

7) Wakuu wa Wilaya wanaobaki katika vituo vyao vya sasa

Wakuu wa Wilaya wafuatao wanaendelea kubaki katika vituo
vyao vya sasa;

JINA JINSIA NA WILAYA

1 Jowika Wilson Kasunga ME Monduli
2 Raymond Hieronimi Mushi ME Ilala
3 Sophia Edward Mjema KE Temeke
4 Bw. Amani Kiungadua Mwenegoha ME Bukombe
5 Bw. Ibrahim Wankanga Marwa ME Nyang’wale
6 Bw. Rodrick Lazaro Mpogolo ME Chato
7 Bw. Manzie Omar Mangochie ME Geita
8 Bi. Darry Ibrahim Rwegasira KE Karagwe
9 Lt. Col. Benedict Kulikila Kitenga ME Kyerwa
10 Constantine John Kanyasu ME Ngara
11 Paza Tusamale Mwamulima ME Mpanda
12 Peter Toima Kiroya ME Kakonko
13 Hadija Rashid Nyembo KE Uvinza
14 Dkt. Charles O. Mlingwa ME Siha
15 Shaibu Issa Ndemanga ME Mwanga
16 Herman Clement Kapufi ME Same
17 Ephraim Mfingi Mbaga ME Liwale
18 Abdallah Hamis Ulega ME Kilwa
19 Joshua Chacha Mirumbe ME Bunda
20 Deodatus Lucas Kinawiro ME Chunya
21 Rosemary Staki Senyamule KE Ileje
22 Gulamhusein Kifu Shaban ME Mbarali
23 Christopher Edward Magala ME Newala
24 Baraka Mbike Konisaga ME Nyamagana
25 Sarah Philip Dumba KE Njombe
26 Hanifa Mahmoud Karamagi KE Gairo
27 Halima Meza Kihemba KE Kibaha
28 Nurdin Babu ME Rufiji
29 Mathew Sarja Sedoyeka ME Sumbawanga
30 Idd Hassan Kimanta ME Nkasi
31 Chande Bakari Nalicho ME Tunduru
32 Bibi Senyi Simon Ngaga KE Mbinga
33 Wilson Elisha Nkambaku ME Kishapu
34 Benson Mwailugula Mpesya ME Kahama
35 Paul Chrisant Mzindakaya ME Busega
36 Georgina Elias Bundala KE Itilima
37 Fatuma Hassan Toufiq KE Manyoni
38 Lt. Edward Ole Lenga ME Mkalama
39 Hanifa Mohamed Selengu KE Sikonge
40 Suleman Omar Kumchaya ME Tabora
41 Mboni Mwanahamis Mgaza KE Mkinga
42 Seleman Salum Liwowa ME Kilindi

Mabadiliko haya yameanza tarehe 18.02.2015 na ninawatakia wote
utendaji kazi mahiri.

Mizengo K. P. Pinda

18.02.2015 WAZIRI MKUU

No comments: