Saturday, February 14, 2015

AFARIKI DUNIA BAADA YA KUINGIA KWENYE BWAWA



Na Steven Augustino,
Tunduru.

KIJANA wa miaka 18 ambaye amefahamika kwa jina la Hamisi Mandanje, amefariki dunia baada ya kuzama katika maji yaliyokuwa yametuama, katika bwawa moja maarufu linalofahamika kwa jina la book wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma.

Taarifa za tukio hilo zinaeleza kuwa marehemu huyo, kabla ya kupatwa na mkasa huo alikwenda katika bwawa hilo kwa lengo la kufua nguo zake.

Akizungumzia tukio hilo, shuhuda ambaye alijitambulisha kwa jina la Mohamed Said alisema, lilitokea majira ya mchana Feburuary 10 mwaka huu.


Baada ya marehemu kumaliza zoezi la kufua nguo zake, alijaribu kuingia ndani ya bwawa hilosehemu ambayo ilikuwa na maji mengi, akidai kuwa anataka kuvuka upande wa pili eneo ambalo shuhuda huyo alikuwa akivua samaki.

 Alisema wakati akiwa katika harakati hizo, ghafla alimuona amezama na kuibuka mara moja na alipozama tena hakuonekana, hadi wapigambizi walipofika kuopoa mwili wake baada ya masaa manne kupita.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma, ASP Mihayo Msikhela amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kuongeza kuwa, Polisi wanendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo.

No comments: