Wednesday, June 10, 2015

MKUU WA SHULE SEKONDARI NANUNGU ADAIWA KUKWAMISHA UJENZI WA MAABARA

Na Mwandishi wetu,
Namtumbo.

MOHAMED Ngonyani, ambaye ni Mkuu wa shule ya sekondari Nanungu kata ya Hanga wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma, analalamikiwa akidaiwa kukwamisha ujenzi wa jengo la maabara kutokana na kuzuia kiasi cha shilingi milioni 1,330,000 ambacho alipaswa kulipa mafundi wanaojenga jengo hilo, licha ya kamati husika ya ujenzi kuidhinisha malipo hayo.

Fedha hizo ni kati ya shilingi milioni 3,500,000 zilizopo katika mkataba wa ujenzi kati ya Mkuu wa shule na fundi mkuu anayesimamia ujenzi huo, George Mbeya akisaidiana na watu wengine ambapo jengo hilo kwa ujenzi wake umesimama kutokana na kuwepo kwacmgogoro huo na limefikia katika hatua ya kuezeka.

Kufuatia hali hiyo Ngonyani ametishia kuchukua hatua dhidi ya kamati husika ya ujenzi, ili kuondoa adha anayoendelea kuipata na kumfanya ashindwe kukamilisha kazi hiyo kwa wakati.


Akitoa malalamiko yake mbele ya waandishi wa habari, alisema makubaliano ya kujenga vyumba vitatu vya maabara yalikuwa ni ya shilingi milioni 3,500,000 na tayari alikwisha pewa shilingi milioni 2,200,000 lakini anashangaa hivi sasa baada ya kumaliza kazi hiyo, anapigwa dana dana na kuzungushwa bila kulipwa fedha yake.

“Inasikitisha kuona yule Mkuu wa shule anaonesha dhahiri anataka kunidhulumu fedha yangu, kila ninapomfuata pale shuleni amekuwa ni mtu wa kunitishia na kunifokea kwa ukali kwa nini naingia maeneo ya shule bila kibali maalum, kwa kweli ananishangaza sana”, alisema George.


Mkuu wa shule ya Sekondari Nanungu, Ngonyani alipoulizwa juu ya madai hayo alikanusha kuhusika na malipo ya fundi huyo na kueleza kuwa yeye hatambui mkataba wa kazi hiyo, huku akiongeza kuwa kazi ya ujenzi wa jengo hilo la maabara alipewa na kamati ya maendeleo ya kata na sio uongozi wa shule hiyo.

No comments: