Saturday, January 28, 2017

NAMTUMBO WAMLALAMIKIA DOKTA MAHENGE GHARAMA ZA KUSAFIRISHA WAGONJWA

Na Yeremias Ngerangera,    
Namtumbo.

WANANCHI wanaoishi katika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma, wamelalamikia gharama za kusafirisha wagonjwa wao kutoka wilayani humo kwenda hospitali ya Rufaa Songea, wakidai kuwa hali hiyo inachangiwa kwa kiasi kikubwa na uongozi wa Manispaa ya Songea mkoani humo kuzuia magari kushusha abiria katika eneo la hospitali hiyo. 

Malalamiko hayo ya wananchi hao yaliwasilishwa mbele ya Mkuu wa mkoa huo, Dkt. Binilith Mahenge katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini hapa juzi, huku wakiongeza kuwa hali hiyo imekuwa ikiwatesa wananchi hao na wagonjwa wanaokwenda kutibiwa katika hospitali hiyo.

Walibainisha kuwa gharama kubwa zipo katika kukodi magari kama vile taxi ambapo madereva wanaoendesha gari hizo huwatoza shilingi 10,000 mpaka 12,000 kutoka stendi kuu Msamala mjini Songea.


Kwa upande wake Dkt. Mahenge aliwataka wananchi hao, kuwa watulivu wakati Ofisi yake inalifanyia kazi ili kuweza kuondoa usumbufu huo wanaoupata sasa.

No comments: