Monday, February 26, 2018

MBUNGE MBEYA MJINI NA MWENZAKE WATUPWA JELA KIFUNGO CHA MIEZI MITANO



Na Mwandishi wetu,

HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, imewatia hatiani Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu na Katibu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya nyanda za juu kusini, Emmanuel Masonga na kuwahukumu kifungo cha miezi mitano jela.

Aidha hukumu hiyo imetolewa leo Februari 26 mwaka huu na Hakimu Mkazi mfawidhi wa Mahakama hiyo, Michael Mteite ambapo Sugu na Masonga wamehukumiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais Dokta John pombe Magufuli.


Wawili hao wanadaiwa kutenda kosa hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Desemba 30 mwaka jana eneo la Uwanja wa shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.

No comments: