Tuesday, February 13, 2018

WAZIRI JAFFO AGOMA KUZINDUA MRADI WA MAJI CHAMWINO DODOMA


Na Mwandishi wetu,

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (TAMISEMI) Seleman Jaffo, amegoma kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Itiso Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma kutokana na baadhi ya wananchi kuharibu kwa makusudi miundombinu hiyo.
Seleman Jaffo.

Akizungumza na wananchi wa kijiji hicho, Waziri huyo alisema kuwa awali mkandarasi aliyekuwa akijenga mradi huo alikuwa akisuasua na kwamba Halmashauri ya Chamwino iliamua kumbadilisha Mhandisi wa maji, ili kuweza kukamilika kwa haraka ujenzi wake na wa kiwango chenye bora.

Imeelezwa kuwa wananchi wa kijiji cha Itiso wamekuwa hawana ushirikiano mzuri na viongozi wao na wale waliokuwa wakijenga mradi jambo ambalo limekuwa likisababisha uwepo wa uharibifu wa miundombinu hiyo ya maji.


Kufuatia hali hiyo alimuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chamwino, Athuman Masasi kusimamia jambo hilo kikamilifu na wale waliohusika kuharibu miundombinu hiyo washughulikiwe haraka.

Pamoja na mambo mengine, naye Mkurugenzi huyo wa Halmashauri hiyo alisema kuwa licha ya Serikali kugharimia kiasi kikubwa cha fedha kujenga mradi huo, lakini wananchi hao ndiyo wamekuwa mstari wa mbele kuharibu miundombinu hiyo ya maji.

No comments: