Sunday, February 11, 2018

SHIRIKA LA MAENDELEO LA PETROLI TANZANIA LATOA MSAADA WA SHILINGI MILIONI 25 KWA HALMASHAURI YA TUNDURU UJENZI KITUO CHA AFYA NAKAYAYA

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma Juma Homera, upande wa kulia akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni 25 kutoka kwa Meneja mawasiliano wa Shirika la Maendeleo la Petroli Nchini (TPDC) Marie Msellemu kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha afya Nakayaya Wilayani humo.

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera, katikati akiwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Chiza Malando aliyekuwa upande kulia wakifurahia mfano wa hundi ya shilingi milioni 25 iliyotolewa na Shirikala Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha afya Nakayaya ambacho kinatajwa mara kitakapokamilika kitasaidia kusogeza huduma karibu za matibabu kwa wakazi wa maeneo yanayozunguka  kituo hicho, upande wa kushoto ni Meneja mawasiliano wa TPDC Marie Msellemu.

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma, Juma Homera akimtembeza Meneja mawasiliano wa Shirika la Petroli Nchini (TPDC) Marie Msellemu maeneo mbalimbali ya ujenzi wa Kituo cha afya Nakayaya Wilayani hapa, ambacho ujenzi wake umeibuliwa na kuanzishwa na Mkuu huyo wa Wilaya kwa kutumia wafadhili wa kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini.
Meneja mawasiliano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Marie Msellemu katikati, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera ambaye ni wa nne upande kushoto na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, Chiza Malando wa tatu upande kulia wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakuu wa idara ya Halmashauri ya wilaya hiyo, mara baada ya TPDC kukabidhi mchango wake wa shilingi milioni 25 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Kituo cha afya Nakayaya Wilayani humo. 
(Picha zote na Gwiji la Matukio Ruvuma)

No comments: