Sunday, February 11, 2018

SERIKALI YA TANZANIA KUJIONDOA KATIKA MPANGO WA KUSAIDIA WAKIMBIZI



SERIKALI ya Tanzania imesema kwamba inajiondoa katika mpango wa Umoja wa mataifa wa kusaidia wakimbizi kuanza maisha mapya katika mataifa yanayowahifadhi.

Tanzania limekuwa eneo salama kwa wakimbizi wengi na sasa inahifadhi zaidi ya wakimbizi 250,000 wa nchi ya Burundi ambao walitoroka mzozo.

Rais Dokta John Pombe Magufuli amesema kwamba taifa lake linajiondoa kutokana na tatizo la usalama pamoja na lile la kifedha.


.Uganda yakana kutaka kuwafurusha wakimbizi wa Burundi
.Tanzania inahifadhi wakimbizi wengi zaidi kutoka Burundi
.Nkurunziza afika Tanzania ziara yake ya kwanza nje tangu 2015

Mwaka uliopita taifa hilo lilisimamisha kwa muda usajili wa wakimbizi wapya na kuwataka wakimbizi wa Burundi kurudi nyumbani, hatua ambayo ilishtumiwa na makundi ya kupigania haki za kibinadamu.

Kitengo hicho cha Umoja wa Mataifa kinasema kuwa kinatuma ujumbe wa ngazi za juu kwa mazungumzo na Serikali ya Tanzania.

Tanzania ndio nchi inayohifadhi wakimbizi wengi zaidi kutoka Burundi kuliko nchi nyingine yoyote ile katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR.

Ripoti hiyo inasema hadi hivi sasa, kuna wakimbizi laki 2 na elfu 41 kutoka Burundi wanaopatiwa makazi nchini Tanzania.

Katika idadi hii kubwa ya watu wanaokimbia nchi yao, UNHCR inasema asilimia 60 ni watoto.

Na ndani ya kipindi cha miezi mitano tu ya mwaka huu wa 2017, wakimbizi 44,487 wamekimbia Burundi na kuingia Tanzania.

UNHCR inasema huu ni mzigo mkubwa kwa Tanzania lakini kwa bahati mbaya, nchi hii haipati fedha za kutosha kuwahudumia wakimbizi na wengine wanaotafuta hifadhi.

Kambi moja kwa mfano ya Nyarugusu ambayo inatajwa kuwa ni moja ya kambi kubwa za wakimbizi duniani, inahifadhi wakimbizi 139,0000 idadi ambayo inapaswa kupunguzwa na kuwagawa wakimbizi katika kambi nyingine.

Lakini hili limeshindikana, ripoti ya UNHCR inasema, na ni kwasababu ya kukosekana kwa ardhi ya kufungua kambi mpya.

Source:BBC

No comments: