Friday, February 9, 2018

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI ATOA AGIZO KWA JESHI LA POLISI NCHINI

Waziri wa mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba.

Na Mwandishi wetu,

WAZIRI wa Mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba amelitaka Jeshi la Polisi hapa nchini kuziachia Pikipiki zote ambazo wamezishikilia kwa muda mrefu, na zile zenye makosa madogo pia waziachie wasikae nazo kwa muda mrefu mpaka zinafikia hatua ya kuwa vyuma chakavu.

Mwigulu alisema yale yenye makosa makubwa kama uhalifu wa kivita, madawa ya kulevya na wale wanaotelekeza wabaki nazo wafanye utaratibu wa kuwapeleka Mahakamani au kuziteketeza, na zile zenye makosa madogo watatue haraka na kuwarudishia wenye zao huku wakiwapatia elimu wamekosea wapi.

“Wapeni masomo wamekosea wapi waelekezeni na waliowabishi warekebisheni lakini tusirundike tukatengeneza vyuma chakavu kwa hivi vitu ambavyo utatuzi wake tunao, tutumie huu mkono kutatua kwa yale ambayo yapo ndani ya mamlaka yetu”, alisema Mwigulu.


Alisema kuwa ipo haja ya vijana sasa kufundishwa zaidi kuhusu sheria ya usalama barabarani, ili kuweza kupunguza ajali za Pikipiki na mrundikano wa Pikipiki katika vituo vya Polisi nchini kwani kila anapopita vituo vya Polisi hukuta Pikipiki ni nyingi na makosa yao ni madogo madogo ambayo yanaweza kutatuliwa.

No comments: