Thursday, February 15, 2018

MKE NA MUME WAKAMATWA CHINA NA DAWA ZA KULEVYA MTOTO ARUDISHWA TANZANIA



Baadhi ya dawa za kulevya.
Na Mwandishi wetu,

WATANZANIA wawili wamekamatwa nchini China, January 19 mwaka huu wakiwa wamemeza dawa za kulevya tumboni kwenye uwanja wa ndege wa Baiyun Guangzhou.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na kupamba na dawa za kulevya nchini, Rogers Siang’a aliwataja watuhumiwa hao ni Baraka S. Malali na Mkewe Ashura H. Mussa ambapo wamekamatwa wakiwa na mtoto wao mdogo mwenye umri wa miaka 2 na miezi 9.

Kamishna Siang’a alisema kuwa baada ya kukamatwa walihifadhiwa kwenye chumba maalum kwa muda, ndipo Baraka alitoa Pipi 47 kwa njia ya haja kubwa huku Ashura akitoa Pipi 82.


Siang’a alieleza kuwa Serikali ya China iliwasiliana na Serikali ya Tanzania kuhusiana na suala la mtoto huyo, ambapo walikubaliana kumrudisha mtoto huyo hapa nchini. 

Mamlaka ya kupambana na dawa za Kulevya ikishirikiana na Ustawi wa Jamii inafanya jitihada za kuwasiliana na ndugu wa watuhumiwa ili kuhakikisha mtoto huyo anakabidhiwa kwa ndugu zake ili aweze kuendelea kupata matunzo.





No comments: