Monday, December 21, 2015

DOKTA MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA MAALIM SEIF IKULU JIJINI DAR ES SALAAM


DAR ES SALAAM.

RAIS Dokta John Magufuli amekutana na kuzungumza na aliyekuwa mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad juu ya mgogoro wa uchaguzi mkuu, wa Rais wa visiwa hivyo unaoendelea kufukuta chini chini.

Mkutano huo baina ya viongozi hao, umefanyika ikiwa ni siku kadhaa tangu Bodi ya MCC kutangaza kusitisha msaada wa dola Milioni 472.8 ambazo ni sawa na takribani Sh trillioni moja, kwa sababu ya mgogoro huo.

Fedha hizo zililenga kusaidia sekta ya nishati ya umeme, hususan ule wa vijijini kwa kuunganisha wateja wapya na kufanya mabadiliko ya kimuundo ya Shirika la ugavi wa Umeme (TANESCO) ili lifanye kazi na kutoa huduma, kwa ufanisi zaidi katika sehemu za uzalishaji, usafirishaji na usambazaji.


Fedha hizo pia zilikusudiwa kusaidia kuanza kwa mpango mkubwa, wa kuboresha sekta ya umeme nchini 2014-2024.

Mazungumzo ya viongozi hao wawili yamehudhuriwa pia na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.

Viongozi hao kwa pamoja wamejadili hali ya kisiasa Zanzibar, na wamaefurahishwa na hali ya usalama na utulivu inayoendelea.

Rais Dokta Magufuli ameamuahidi Maalim Seif kwamba, mazungumzo yataendelea hadi suluhisho la kisiasa litakapopatikana.

No comments: