Sunday, December 27, 2015

MWENYEKITI CCM MKOA WA IRINGA NA WENGINE WALIOTAJWA KUKISALITI CHAMA WAKATI WA UCHAGUZI MKUU KUANZA KUHOJIWA

Jesca Msambatavangu.

IRINGA.

KAMATI za Maadili Chama cha Mapinduzi (CCM) ngazi mbalimbali mkoani Iringa zinaanza kukutana leo Jumatatu Desemba 28, kusikiliza ushahidi toka kwa wanaCCM wanaodaiwa kukisaliti chama hicho wakati wa uchaguzi Mkuu ambao ulifanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Mmoja wa watakaoitwa na kamati hizo ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo, Jesca Msambatavangu na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa, Mahamudu Madenge.


Msambatavangu na Madenge wanatuhumiwa pamoja na wasaliti wengine 30 wa mjini Iringa, kukisaliti na kukihujumu chama hicho hadi kikapoteza ubunge kwa mara nyingine tena kwa Mchungaji Peter Msigwa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kikanyang’anywa kata 14, walizokuwa wakizishikilia CCM kwa miaka yote.

Kwa upande wake, Msambatavangu ambaye mara kwa mara amenukuliwa akipinga kuhusika katika tuhuma hizo, amesema yupo tayari kutoa ushirikiano kwa kamati hizo na akawataka watuhumiwa wengine wafanye hivyo, ili kumaliza suala hilo linalozidi kukigawa chama hicho mkoani humo.

No comments: