Saturday, February 27, 2016

ITS MY FAULT SASA IPO SOKONI WADAU WATAKIWA KUUNGA MKONO




Na Kassian Nyandindi,

Mbinga.

KWA mara ya kwanza vijana waigizaji kutoka wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma, wameweza kutoa filamu yao mpya yenye picha kali ambayo inatamba mtaani kwa jina la “IT’S MY FAULT” hivyo wadau mbalimbali, wametakiwa kukaa mkao wa kula na kuipokea albamu hiyo kwa kuendelea kuwaunga mkono wasanii hao kwa kazi hiyo waliyoifanya.
Erick Kapinga.

Filamu hiyo imebeba maudhui mazuri, yenye kulenga kuelimisha jamii ikiwa na picha nzuri zenye ubora unaokubalika.

Kazi kubwa ya ‘Production’ ya filamu hiyo, imefanywa na kijana mmoja maarufu mkazi wa Mbinga mjini anayefahamika kwa jina la Erick Kapinga, akishirikiana na timu ya vijana wenzake  kadhaa.

Vijana hao kwa ujumla wameweza kuanzisha kampuni yao ya filamu inayotambulika kwa jina la, Amaizing Films Company (AFC) iliyopo mjini hapa.


Wasanii walioshiriki katika filamu hiyo ni Neema Mwisho, Alhaji Ramadhani, Daniel Nkoma, Notugela David, Faraja Komba, Baraka Chaula, Rose Komba, Richard Mteta na Sarah Komba maarufu kwa jina la Dokela wote wakazi wa Mbinga mjini.

Kwa mtu yeyote ambaye anahitaji kupata filamu hiyo, ambayo sasa ipo sokoni inauzwa kwa gharama nafuu, anaweza kufanya mawasiliano nao kwa kupiga simu ya kiganjani namba 0763 008862.

No comments: