Saturday, February 20, 2016

WANANCHI WATAKIWA KUJIKINGA NA MAGONJWA YALIYOSAHAULIKA

Wakurugenzi na viongozi wa kutoka katika Halmashauri za mkoa wa Ruvuma, wakishiriki semina ya kampeni ya kumeza vidonge kwa magonjwa yaliyosahaulika mjini Songea.
Na Mwandishi wetu,

Songea.

WANANCHI wanaoishi katika mkoa wa Ruvuma na nje ya mkoa huo, wametakiwa kujikinga kwa kujenga mazoea ya kumeza dawa, ambazo huzuia kuenea kwa magonjwa yaliyosahaulika.
 
Imeelezwa kuwa endapo watazingatia hilo, wataweza kuepukana na magonjwa ya matende, usubi, kichocho, trakoma na minyoo.

Mratibu wa magonjwa hayo hapa nchini, Dkt. Edward Kirundi aliyasema hayo mjini hapa na kuongeza kuwa magonjwa hayo  yanatibika, na kwamba jambo muhimu kila mtu anapaswa kuzingatia tiba au kinga.

Vilevile alisisitiza kwa kuitaka jamii hapa nchini, kushiriki kikamilifu katika kampeni ya kutokomeza magonjwa hayo na wataalamu wa afya wazingatie kutoa elimu sahihi kwa wananchi, ili kuifanya jamii iweze kuwa na uelewa juu ya madhara yatokanayo na magonjwa hayo.

No comments: