Thursday, November 9, 2017

MAKAMU WA RAIS AFUNGA KILELE CHA MAADHIMISHO MTANDAO WA POLISI WANAWAKE TANZANIA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akikagua gwaride maalum la Polisi wanawake kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka kumi ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yaliyofanyika kwenye chuo cha taaluma ya Polisi, Kurasini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akipata maelezo juu ya umuhimu wa alama za barabarani kutoka kwa Koplo Faustina Ndunguru wa kitengo cha usalama barabarani makao makuu ya Polisi Dar es Salaam wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka kumi ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yaliyofanyika kwenye chuo cha taaluma ya Polisi, Kurasini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akipata maelezo juu kamera kugundua wanaoendesha kwa mwendo kasi kutoka kwa Konstabo Sharifa Ismail wa kitengo cha usalama barabarani makao makuu ya Polisi Dar es Salaam wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka kumi ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yaliyofanyika kwenye chuo cha taaluma ya Polisi, Kurasini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka kumi ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yaliyofanyika kwenye chuo cha taaluma ya Polisi, Kurasini Dar es Salaam. (Picha zote na Ofisi ya Makamu wa Rais)

No comments: