Tuesday, May 12, 2015

STENDI FC TUNDURU YATAWAZWA KUWA BINGWA WA PEACE AND LOVE

Na Mwandishi wetu,
Tunduru.

TIMU ya Stendi FC Tunduru mjini mkoani Ruvuma, imetawazwa kuwa bingwa ligi ya kuitangaza Hoteli mpya ya Peace and Love iliyopo mjini hapa, baada ya kuwachapa magoli mawili kwa moja, mahasimu wao wa timu ya Usalama FC ya mjini humo.

Mchezaji Shaban Chitepete, ndiye aliyefungua milango ya wapinzani hao baada ya kuifungua timu yake kwa goli la kwanza ambalo lilitikisa nyavu za wapinzani wao katika dakika, ya 21 huku la pili likigonga tena nyavu hizo kwa dakika ya 23 ambalo lilifungwa na Exavia Chimgege, mchezo ambao ulikuwa ukisakatwa katika uwanja wa Chama Cha Mapinduzi mjini Tunduru.

Upande wa usalama FC goli la kufuta machozi lilifungwa na Fakihi Maliyatembo, katika dakika ya 39na kuwahadaa walinzi wa Stendi FC baada ya kufyatua mkwaju mkali, ambao ulimwacha golikipa wa timu hiyo njia panda.

Akizungumzia juu ya mashindano hayo, Mwenyekiti wa Chama cha mpira wa miguu (TDFA) wilaya ya Tunduru, Kitwana Mzee alisema ligi hiyo ambayo ilianza Aprili 9 mwaka huu kwa kushirikisha timu 12 kutoka ndani ya wilaya hiyo.


Kitwana aliendelea kufafanua kuwa, katika mashindano hayo timu hizo ziligawanywa katika makundi mawili A na B huku wakicheza kwa mtindo wa mtoano ambapo katika hatua ya awali, timu sita ndizo zilizofanikiwa kuingia katika awamu ya pili na kupangwa kucheza katika mpango wa mzunguko huo.

Alisema kupitia utaratibu huo, timu nne za kutoka katika kila kundi zilifanikiwa kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho na kuingia nusu fainali na hatimaye timu hizo ambazo zilicheza fainali hiyo.

Sambamba na hayo, Stendi FC waliibuka kidedea kwa kuzoa kitita cha shilingi 150,000 kikombe na seti moja ya jezi, mshindi wa pili ni Usalama FC ambao nao waliambulia shilingi 150,000 na seti moja ya jezi wakati mshindi wa tatu Jeboyebo FC walinyakua shilingi 100,000 na mpira mmoja.

Timu nyingine ambazo zilishiriki katika ligi hiyo kuwa ni; Tunduru star FC, Majengo FC, Liver Combain FC, Tiger FC, Joka FC, Mambo mazuri FC, Veteran FC, Jobe FC na Red Scorpion FC na kwamba mgeni rasmi katika mashindano hayo alikuwa ni Katibu tawala wa wilaya ya Tunduru, Ghaibu Lingo.


Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Alli Mpenye alisema katika awamu ya kwanza zoezi hilo lilihusishwa katika kata tano za Mgombasi ambapo watu waliojiandikisha walikuwa 5,186, Namtumbo 9,041, Likuyu 4,952, Rwinga 7,586 na kata ya Luegu watu waliojiandikisha walikuwa 4,064.

Mpenya alifafanua kuwa hivi sasa wanaendelea na kata nyingine, na kwamba wamelazimika kufanya kwa wamu kutokana na ufinyu wa vifaa ikiwemo mashine ya kuandikishia wapiga kura (BVR) ambapo baadhi yake zilizoletwa na tume ya taifa ya uchaguzi ni mbovu na hushindwa kufanya kazi ipasavyo na kulazimika kutumia mashine chache zilizopo ambazo hufanya kazi.

Alieleza kuwa baada ya kumaliza kazi hiyo ya uandikishaji katika kata hizo, zoezi hilo litaendelea tena katika kata ambazo zipo pembezoni mwa wilaya hiyo ambazo ni Ligera, Lusewa, Mgazini na kata ya Msisima.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, awali kazi hiyo ilianza kwa kusuasua kwa kile alichoeleza kuwa mwitikio mdogo wa wananchi wenyewe na baada ya kuwafikia taarifa za bkutosha katika maeneo yao ndipo walianza kujitokeza kwa wingi.

Asasi za kiraia, wananchi na vyama vya siasa, Mpenye amevipongeza kwa jitihada yao ya kupita kuhamasisha zoezi hilo ili watu wakajiandikishe na ndio maana wengi wao hivi sasa katika vituo husika wilayani humo, wanahamasa kubwa ya kutekeleza zoezi hilo ili utakapofika uchaguzi mkuu ujao waweze kupiga kura na kumchagua kiongozi wanayemataka awaongoze, kwa nafasi ya Rais, Mbunge na Diwani.



No comments: