Friday, May 1, 2015

WATAKIWA KUPELEKA WATOTO WAO KWENYE CHANJO

Na Mwandishi wetu,
Tunduru.

WANANCHI wilaya ya Tunduru mkoani hapa, wamehimizwa kupeleka watoto wao katika vituo vya kutolea huduma za afya ili waweze kupatiwa chanjo za magonjwa pingamizi, katika ukuaji wa watoto hao.

Chande Nalicho alitoa rai hiyo wilayani humo, wakati wa zoezi la uzinduzi wa wiki ya utoaji wa chanjo duniani, ambalo Tunduru lilifanyika katika viwanja vya hospitali ya serikali ya wilaya hiyo.

Aidha Mkuu huyo wa wilaya, aliwataka akina mama ambao walijitokeza katika zoezi hilo kuwa wajumbe wa kusambaza taarifa kwa wenzao, ili kuweza kuhamasisha jamii iweze kujitokeza kwa wingi na kupatiwa huduma hiyo.


Pamoja na mambo mengine, akisoma taarifa ya uzinduzi wa siku ya chanjo duniani katibu wa afya wilayani Tunduru, Maria Mzena alisema kuwa chanjo hizo ni muhimu hivyo jamii inapaswa kushiriki kikamilifu.


Mratibu wa chanjo wilaya ya Tunduru, Rozi Jemeni alisema kwamba mwaka huu idara yake imejipanga na kuhakikisha kuwa inatekeleza zoezi hilo, kwa asilimia 100 ikiwa ni tofauti na chanjo zilizofanyika mwaka jana ambapo wilaya ilichanja watoto kwa asilimia 93 tu.

No comments: