Friday, May 29, 2015

WATENDAJI TUNDURU WATAKIWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO

Na Mwandishi wetu,
Tunduru.

SERIKALI wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma, imewaagiza watendaji wote wa vijiji wilayani humo kuhakikisha kwamba wanasimamia na kutekeleza ipasavyo sheria ndogo ndogo, ambazo zimetungwa na kupitishwa na baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya hiyo.

Aidha wameagizwa kuacha vitendo vya ulegevu, wakati wanapotekeleza majukumu yao ya kazi na kusababisha mwanya kwa wananchi kuvunja sheria husika, hatimaye maendeleo kushindwa kusonga mbele.

Katibu tawala wilayani Tunduru, Ghaibu Lingo alitoa agizo hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Matemanga wilayani humo.


“Watendaji ambao mnajiona hamna uwezo wa kutekeleza majukumu mliyopewa na serikali, ni muda muafaka sasa mkajiondoa wenyewe kwa kufuata taratibu za kiutumishi ili muweze kuwapisha wengine, ambao wapo tayari kulitumikia taifa hili”, alisema Lingo.


Alisema haiwezekani serikali iendelee kumfumbia macho mtendaji ambaye hatekelezi majukumu yake ipasavyo, na kuiacha jamii ikivunja sheria na taratibu zilizowekwa kwa makusudi au bila kujua hatimaye kusababisha hasara kwa wananchi wengine.

No comments: