Sunday, November 15, 2015

HATIMAYE MIILI YA MAREHEMU WALIOUAWA LEO KIKATILI YAZIKWA KATIKA MAKABURI YA MISHENI MBINGA


Na Mwandishi wetu,

Mbinga.

HATIMAYE miili ya watoto wawili waliouawa kikatili kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na mkazi mmoja wa kijiji cha Zomba wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, Dickson Lupogo (28) imezikwa leo katika makaburi yaliyopo mtaa wa Misheni mjini hapa.

Watoto hao wawili ambao walipoteza maisha katika tukio hilo ni, Lulu Chang’a (14) na Furaha Ndunguru (7) ambaye ni wa darasa la kwanza shule ya msingi Nyerere iliyopo mjini hapa, na kwamba mazishi hayo yamefanyika majira ya saa 11:30 katika makaburi ya mtaa wa Misheni.

Kadhalika Dickson Lupogo ambaye ndiye aliyefanya unyama huo, na mwili wake kuchomwa moto na watu wenye hasira kali na kupoteza maisha, naye amezikwa kijijini kwao Zomba, baada ya ndugu zake kuwasili katika Hospitali ya wilaya hiyo na kuuchukua mwili wake.


Hali kadhalika mtoto Moses Ndunguru (3) aliyejeruhiwa vibaya, amesafirishwa kwenda Hospitali ya Misheni Peramiho iliyopo wilaya ya Songea mkoani humo, kwa matibabu zaidi kutokana na hali yake kuwa mbaya.

Mwandishi wa habari hizi aliwasili eneo la tukio, majira ya asubuhi leo Novemba 15 mwaka huu, na kushuhudia mauaji hayo yaliyofanyika mtaa wa Tangi la maji A Mbinga mjini.

Hata hivyo Polisi wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo, ili kuweza kubaini chanzo chake.

No comments: