Thursday, November 5, 2015

MAGUFULI AANZA KAZI AMTEUA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI



Na Waandishi wetu,

Dar.

SAA chache baada ya kuapishwa rasmi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Magufuli ameanza kazi kwa kasi ambapo leo ameanza kwa kumteua mwanasheria Mkuu wa serikali yake ya awamu ya tano, na kuitisha bunge.

Akizungumza na waandishi wa habari, kwa niaba ya serikali katika viwanja vya Ikulu Jijijini Dar es salaam Katibu mkuu kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amesema Rais Magufuli ameanza kazi leo hii kwa kumteua Mwanasheria mkuu wa serikali ambaye ni, George Mcheche Masaju aliyewahi kushikilia nyadhifa hiyo katika serikali ya awamu ya nne chini ya uongozi wa Rais mstaafu, Dokta Jakaya Mrisho Kikwete.


Mwanasheria huyo mteule, anatarajia kuapishwa kesho saa nne asubuhi Novemba 6 mwaka huu, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali.

Hata hivyo, Balozi Sefue ameeleza kuwa Rais Magufuli ameitisha Bunge la 11 ambalo litafunguliwa rasmi Novema 17 hadi 19 mwaka huu, wakati huo Rais atakuwa amependekeza pia jina la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa serikali ya awamu ya tano na kusubiri ridhaa ya wabunge.

No comments: