Friday, November 6, 2015

MWALIMU AKUTWA KWENYE MTARO AKIWA AMEFARIKI DUNIA



Na Kassian Nyandindi,
Songea.

HENRY Millinga (34) ambaye ni mwalimu wa shule ya sekondari Msamala katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, amefariki dunia na mwili wake ukiwa umetupwa
ana mjini Songea na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Mihayo Msikhela zimeeleza kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Novembkwenye mtaro wa maji machafu.

Katika tukio hilo imeelezwa kuwa pembeni ya mwili wa mwalimu huyo, amekutwa akiwa na vipande vya chupa za bia, huku katika paji lake la uso akiwa na majeraha makubwa.

Habari zilizopatika 5 mwaka huu, katika eneo la Nane nane lililopo Msamala mjini hapa.

Inadaiwa siku ya tukio hilo, Mkuu wa Polisi wilaya ya Songea alipokea taarifa kutoka kwa raia wema kwamba huko katika eneo la Nane nane Msamala kuna mtu mmoja ameonekana akiwa ametupwa katika mtaro wa maji machafu na amepoteza fahamu, ndipo jitihada za Polisi kufika eneo la tukio zilifanikiwa na baadaye kwenda katika eneo hilo kumkuta mtu huyo akiwa ndani ya mtaro huo amefariki.

Kamanda Msikhela alieleza kuwa askari Polisi wakiwa kwenye eneo la tukio, huku umati mkubwa wa watu wakijitokeza kushuhudia ndipo baadhi yao waligundua kuwa mwili wa marehemu huyo, ni mwalimu wa shule ya sekondari Msamala.


Baada ya kubaini hilo alitafutwa Mkuu wa shule hiyo ya sekondari, Irine Chitinde ambaye alithibitisha kuwa ni mwalimu mwenzake Henry Milinga, mkazi wa eneo moja maarufu la kwa Gasa katika Manispaa ya Songea.

Polisi walifanya jitihada ya kuuchukua mwili wake, na kuupeleka Hospitali ya serikali ya rufaa mkoa wa Ruvuma iliyopo katika Manispaa hiyo, ambako ilithibitishwa kuwa Milinga alikuwa ameshafariki dunia kutokana na kuvuja kwa damu nyingi katika jeraha alilokuwa nalo kwenye paji la uso.

Uchunguzi wa awali Polisi imebaini Milinga katika uhai wake, alikuwa akipendelea kunywa katika baa moja maarufu ya Mtini iliyopo mjini hapa na kwamba inahofiwa kuwa mauti yalimkuta wakati akiwa anarudi nyumbani kwake, na Polisi bado inaendelea kufanya uchunguzi zaidi ili kubaini chanzo cha kifo chake.

No comments: