Thursday, November 5, 2015

USINYANYASWE NDUGU FANYA HAYA UWAPO MIKONONI MWA POLISI



IMEANDALIWA  NA  MAWAKILI WETU

( 1 )Askari  akikuweka   chini ya ulinzi  muulize  kitambulisho  ni  haki yako.

( 2 )Askari akikukamata akuoneshe  kitambulisho chenye muhuri wa mahakama  kama anasema ametumwa na mahakama kukukamata, ni haki yako.

( 3 )Askari akikukamata akwambie kwa nini anakukamata  na anakupeleka kituo gani, ni haki yako.

( 4 )Unaruhusiwa  na ni sheria kukataa kukamatwa hata kutumia nguvu kama hukuambiwa  sababu  ya  kukamatwa.

( 5 )Askari anapokiuka taratibu za ukamataji anageuka na kuwa  mhalifu  ni haki  yako kujikinga naye.


( 6 )Askari haruhusiwi  kukuvuta shati, kukukaba koo, kukushika suruali kama hujakataa kutii amri  halali.

( 7 )Askari haruhusiwi kuondoka  na mtu mwingine baada ya kumkosa mtuhumiwa  halisi.

( 8 )Askari  haruhusiwi  kupekua nyumba ya mtu bila kibali  cha kupekua.

( 9 )Askari lazima akuoneshe kibali cha kupekua na ukisome.

( 10 )Kibali kieleze jina la aliyekitoa, kituo kilipotolewa, jina la mtu au sehemu ya upekuzi au uchanganuzi wa mtu au sehemu.

( 11 )Hairuhusiwi  kupekuliwa usiku kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 12 asubuhi.

( 12 )Ni  haki yako kumpekua askari kabla  hajakupekua ili asipandikize kitu.

( 13 )Usipekuliwe nyumbani bila kuwapo kiongozi  wa mtaa.

( 14 )Kila kitakachochukuliwa katika upekuzi lazima kiandikwe na askari aweke sahihi.

( 15 )Mali iliyochukuliwa  katika upekuzi lazima ibaki salama.

( 16 )Mwanaume haruhisiwi kumpekua mwanamke na mwamke haruhusiwi kwa mwanaume.

( 17 )Unaruhusiwa  kukataa kupekuliwa iwapo taratibu hizi hazikufuatwa.

( 18 )Askari haruhusiwi kukutukana wala kukupiga.

( 19 ) Unaruhusiwa kutozungumza lolote mpaka unayemuamini afike uwapo chini ya ulinzi, ni haki yako.

( 20 )Usilazimishwe kuongea au kuandika ambacho hutaki, ni haki yako.

( 21 )Usitoe maelezo bila uhakika yatatumika mahakamani yatakuletea shida.

( 22 )Unaruhusiwa kukaa kimya na usizungumze kitu  uwapo chini ya ulinzi.

HIZI  ZOTE  NI  HAKI  ZAKO, ZILAZIMISHE    USIBEMBELEZE  WALA    USIZIOMBE.  

(Kwa hisani ya sheriayakub.blogspot.com)

No comments: